METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, September 19, 2020

CRDB YAWAFUNDA MAWAKALA WAKE WA MIPAKANI KUHUSU UTAKATISHAJI FEDHA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya CRDB wa mkoa wa Kilimanjaro ,mafunzo yaliyofanyika katika mji mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro.Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB mkoa wa wa Kilimanjaro walioshiriki katika mafunzo ya siku Moja yaliyofanyika katika Hoteli ya Africn Flower iliyopo mji Mdogo wa Himo mkoani Kilimanjaro Meneja wa CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa mafunzo kwa Mawakala wa Benki hiyo yaliyofuguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira (kulia kwake) wengine katika picha ni Donat Mushi (kushoto) Meneja Mwandamizi wa CRDB Wakala na kulia ni Goodluck Ruhago ,Meneja Ufanisi wa Wakala kutoka CRDB Makao MakuuBaadhi ya Mawakala wakifuatilia kwa karibu mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na maafisa kutoka CRDB Makao Makuu na Kanda ya Kaskazini Meneja Mwandamizi -CRDB WAKALA ,Donat Mushi akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo juu ya masuala ya usalama wakati wa utekelezaji wa majukumu yao kama mawakala wa CRDB Meneja Ufanisi wa Wakala kutoka CRDB Makao Makuu ,Goodluck Ruhago akiwaeleza jambo washiriki wa mafunzo hayo yaliyohusisha Mawakala kutoka maeneo mablimbali ya mkoa wa Kilimanjaro .Baadhi ya Mawakala wa Benki ya CRDB mkoa wa Kilimanjaro Meneja Mawakala Kanda ya Kaskazini ,Judica Kweka akizungumza wakati wa mafunzo hayo Baadhi ya Mawakala wa CRDB walioshiriki katika mafunzo hayo Baadhi ya Mawakala wa CRDB mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira na viongozi wa CRDB Kanda ya Kaskazini muda mfupi baada ya kufungua mafunzo kwa Mawakala hao.

Zaidi ya Mawakala 50 wa Benki ya CRDB katika mkoa wa Kilimanjaro wakiwemo wanaofanya shughuli zao katika mpaka wan chi jirani ya Kenya wamepewa mafunzo juu ya tahadhari na kujiepusha na matukio ya utakatishaji fedha . 

Mafunzo hayo yaliyotolewa na maofisa kutoka CRDB Makao makuu na Kanda ya Kaskazini yametolewa kwa mawakala kutoka maeneo ya Mwanga ,Himo ,Marangu ,Rommbo Mkuu,Tarakea na Holili ikiwa ni muendelezo wa mafunzo yanayofanyika nchi nzima . 

Akifungua mafunzo hayo katika Hoteli ya African Flower iliyopo mji mdogo wa Himo ,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Dkt Anna Mghwira alisema ni rahisi kwa wahalifu kujaribu kuwatumia . 

“Kupitia mafunzo haya mazuri mtaweza kupewa elimu ya kumtambua mteja wako na kumuhudumia ipasavyo na kukuwezesha kulinda na kukuza mtaji wako uweze kufanya kazi vyema zaidi.” Alisema Dkt Mghwira . 

Alisema uwakala wa Kibenki umefungua Fursa nyingi na kuwezesha kukua kwa uchumi na kwamba serikali inajivunia uwepo wa mawakala kwa kufungua milango ya urahisi wa kukusanya kodi kwa kuwezesha wananchi kulipia kodi popote alipo kwa Wakala wa CRDB. 

“Wakala wa CRDB ni moja ya njia zinazoongoza kupendwa na wananchi kulipia kodi ambapo naambiwa zaidi ya miamala millioni 8 yenye thamani zaidi ya Bil 300 zilikusanywa kupitia wakala wa CRDB kwa Mwaka Jana tu.”alisema Dkt Mghwira 

“Na kwa nusu ya mwaka huu tayari mmesaidia serikali kukusanya  zaidi ya Bil 350..hii ni kidhihirisho kwamba uwakala wa CRDB ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya Taifa kwa ujumla.”aliongeza Dkt Mghwira . 

Naye Meneja wa CRDB kanda ya Kaskazini ,Chiku Issa alisema  CRDB ndio benki ya kwanza kuanzisha huduma za mawakala wa benki ambazo ilianzisha mwaka 2013 na kwamba kwa sasa ina mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania nzima. 

“Moja ya lengo la kuandaa semina hii  ilikuwa kuwashukuru mawakala hao katika kutambua mchango wao katika kukubali kushirikiana na benki ya CRDB katika kupeleka huduma karibu na wateja lakini pia kuwajumuisha wananchi kwenye huduma za kifedha (financial inclusion)”alisema Chiku 

Alisema mawakala wa  CRDB wamesaidia kuongeza huduma za kibenki kwa kuongeza muda wa wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala wanatoa huduma kwa masaa 24. 

“Mafunzo haya yamelenga pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na kanuni zote za kifedha kama zinavyosimamiwa na benki kuu. Lakini pia wamepewa elimu kuhusiana na elimu ya utakatishaji Fedha.”alisema Chiku. 

CRDB imetoa elimu ya ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia wateja wa benki, pamoja na kusaidia kuongeza wateja ili wananchi waendelee kufurahia huduma zetu lakini pia na mawakala waweze kujipatia kipato zaidi. 

Mwisho

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com