Mkuu wa
Wilaya ya Arusha Mhe Kenani Kihongosi akizungumza na Maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Arusha
na nje ya Wilaya hiyo, waliojitokeza katika Tamasha la “Arusha Festival”
lililoandaliwa na ofisi yake
Maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Arusha na nje ya Wilaya hiyo, waliojitokeza katika Tamasha la “Arusha Festival” lililoandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Kenani Kihongosi wakifuatilia tamasha hilo.
Na Innocent Natai
Akifungua tamasha hilo lililokuwa
na lengo la kuonyesha fursa za burudani na uchumi kwa wasanii na wananchi wa
Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Kenani Kihongosi ambae ndie aliyefungua na kufunga
tamasha hilo amewahakikishia wakazi wa Arusha Kuwapa ushirikiano zaidi na
kuibua vipaji vipya na kuviendelea kwani sanaa ni Ajira
Aidha Dc Kenani amewataka
wakazi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuzidi kuiunga mkono serikali ya awamu
ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli iliyofanya na
inayozidi kufanya mambo makubwa katika sekta ya sanaa na burudani kwa ujumla ambayo pia imelenga kuendeleza sanaa hapa
nchini na kuwafanya wasanii kufaidika na sanaa zao.
Dc Kenani amesema ni dhamira
ya ofisi yake kuhakikisha Wilaya ya Arusha inakuwa Wilaya ya mfano kwa kuwa na
maendeleo,usalama na amani huku pia wananchi wake wanaofanya sanaa mbalimbali wakizidi kuendeleza vipaji
vyao kupitia matamasha mbalimbali kama lililoandaliwa na Ofisi yake ili wanufaike na Sanaa
zao
Aidha Wananchi wa Arusha wamepongeza Ubunifu huo na wameipongeza
serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe rais Dkt JOHN POMBE MAGUFULI kwa kuwajali Vijana na
kuweka historia Isiyofutika Katika Wilaya ya Arusha kwa uwepo wa Tamasha Hilo.
Tamasha La Arusha festival lililoandaliwa na Ofisi Ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Kenani Kihongosi lililohudhuriwa na Maelfu ya wakazi wa Viunga vya Jiji la Arusha na hata nje ya Jiji hilo limefanyika katika viwanja vya Soko la Kilombero huku lilitumbuizwa na wasanii Maarufukutoka Mkoa wa Arusha na nje wakiwemo Dipper Rato,Dogo Janja,Marioo,Beka Flavour,Kala Jeremiah,Baraka The Prince,Meda Classic na wengine lukuki.
0 comments:
Post a Comment