Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiongea na Menejimenti
ya Wizara kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kilimo IV Wizarani Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akiwa pamoja
na Manaibu Waziri wa Wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri Mhe. Hussein Bashe na
Kulia ni Naibu Waziri Mhe.Omary Mgumba wakiwa katika kikao cha menejimenti ya
Wizara.
Waziri wa
Kilimo Japhet Hasunga amewaagiza watendaji Wakuu wa wizara na taasisi zake
kuhakikisha wanasimamia kikamilifu uzalishaji wa mazao na upatikanaji wa masoko
ya uhakika.
Ametoa
kauli hiyo leo (05 .06.20200 alipofanya kikao kazi cha menejimenti iliyohusisha
wakurugenzi wa wizara,bodi za mazao na wakala zilizo chini ya wizara hiyo
jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa kazi za wizara.
Hasunga
amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano ya serikali ya awamu ya tano
wizara ya Kilimo imefanikiwa kuimarisha uzalishaji wa mazao hususan ya chakula
hali iliyopelekea nchi kuwa na utoshelevu wa chakula kipindi chote.
“ Wizara ya
Kilimo imefanya mengi ya manufaa kwa
kusimamia wakulima kuzalisha mazao mengi ya chakula na biashara hali
iliyopelekea uchumi wa nchi kuimarika “ alisisitiza Waziri Hasunga
Katika
kikao hicho cha mwisho katika mwaka mwa fedha 2020 Waziri Hasunga alisema watendaji Wakuu wa wizara Taasisi
watapimwa kwa kuongeza uzalishaji mazao ya kilimo ,pili idadi ya ajira
zitakazozalishwa kwenye mnyororo wa thamani wa zao,
Tatu
mchango wa zao katika upatikanaji wa fedha za kigeni, na nne idadi ya wakulima
na kiasi cha ekari wanachozalisha.
Hasunga
aliongeza kuwa Bodi za mazao zitapimwa kwa mashamba bora ya mfano
waliyonayo,sita idadi ya viwanda vinavyochakata mazao ya Kilimo na mwisho idadi
ya masoko kwa mazao ya wakulima.
Amezielekeza
bodi za mazao na taasisi zote kuhakikisha zinaweka utaratibu mzuri wa kuepusha
kero za wakulima kuhusu upatikanaji wa mbegu bora,pembejeo,viuatilifu na masoko
ili wanufaike na kazi za Kilimo .
“Rais Dkt.
John Pombe Magufuli ameagiza wizara ya Kilimo kuhakikisha inaondoa kero zote za
wakulima kwa kuzitatua haraka katika ngazi zote hadi wilayani ili asiwepo mtu yeyote
atakayekuwa kikwazo kwa wakulima nchini” amesisitiza Waziri Hasunga.
Katika
kikao kazi hicho Waziri huyo wa amesisitiza kuwa serikali haitopanga bei za
mazao ya pamba,mahindi mpunga au ufuta bali itahakikisha wakulima wanapata bei
nzuri ya soko.
Kwa upande
wake Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya amesema watumishi na watendaji
wa wizara wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ubunifu ili
wakulima nchini wanufaike .
Kusaya
alisema ataendelea kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa watendaji wakuu na
taasisi zake ili malengo ya Serikali na maagizo yote yapatiwe utekelezaji ili
uzalishaji na tija kwa mazao ya wakulima nchini uongezeke.
Kikao kazi
hicho kimehudhuriwa pia na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba ambao
wametumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi kwa ushirikiano walioutoa kwa
Mawaziri kwa kipindi chote walichofanya kazi wizarani hapo.
0 comments:
Post a Comment