Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu
akisoma hotuba kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani
leo Juni 5, 2020 jijini Dodoma yaliyoambatana na ufungaji na utoaji vyeti kwa wakaguzi
wa mazingira kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa za Mkoa wa Dodoma. Kaulimbiu
ya mwaka huu ni “Tutunze Mazingira: Tukabiliane na Mabadiliko ya Tabianchi”.
Wengine pichani kulia ni Katibu Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Balozi Joseph Sokoine.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu
akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Wakaguzi wa Mazingira katika Siku ya
Mazingira Duniani leo tarehe 05 Juni 2020.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu
akitoa cheti cha kuhitimu mafunzo ya wakaguzi wa mazingira kwa Mamlaka za
Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma kwa Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Mpwapwa, Theodory Mulokozi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku
ya Mazingira Duniani leo Juni 5, 2020 jijini Dodoma.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Azzan Zungu amesema suala la mabadiliko
ya tabianchi halitambui mipaka ya kijiografia wala ya kisiasa, hivyo, juhudi za
kukabiliana na changamoto hii zinahitaji ushirikiano wa pamoja baina ya Jumuiya
za Kimataifa.
Hayo
ameyasema hii leo Jijini Dodoma katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani
ambapo ameitaka jamii ya watanzania kuendelea kulinda mazingira kwa mustakabali
wa maendeleo endelevu.
Amebainisha
kuwa nchi yetu ni Mwanachama wa Jumuiya za Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira
za kikanda na za Kidunia, hivyo inatekeleza Sera na Sheria za mazingira
kuendana na makubaliano na maazimio yanayofikiwa katika Jumuiya hizo kwa kadri
inavyowezekana.
“Nchi yetu
ni Mwanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi
unaojulikana kama Mkataba wa kulinda mazingira wa Paris (Paris Agreement). Katika kutekeleza Mkataba huu, Nchi
wanachama zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa gesijoto kwa pamoja na kuongeza
juhudi za kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi” Zungu alisisitiza.
Amesema
kuwa Tanzania imeandaa miradi ya kimkakati kwa lengo la kupunguza uzalishaji wa
gesijoto ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge) na
ujenzi wa bwawa la uzalishaji wa umeme wa megawati 2115 (Mwalimu Nyerere
Hydropower – Stieglers Gorge).
“Malori na
mabasi hutumia dizeli ambayo huzalisha gesijoto aina ya hewa ukaa. Reli
ya kisasa inayojengwa haitatumia dizeli bali itatumia umeme ambao unatokana na
nguvu ya maji, pia kwa kujenga bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere tutaongeza
kiasi kikubwa cha umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji, na kupunguza kwa kiasi
kikubwa matumizi ya gesi asilia na dizeli katika uzalishaji wa umeme” Zungu
alisisitiza.
Amebainisha
kuwa umeme wa uhakika utakaozalishwa na Bwawa la Mwalimu Nyerere utasaidia
wananchi walioko vijijini na mijini kupata nishati ya uhakika na kwa gharama
nafuu na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa ukataji wa miti kwa ajili ya kupata
nishati ya kuni na mkaa. Jitihada hizi zitachangia kwa kiasi kikubwa kwenye
hifadhi ya mifumo asilia ya kimaumbile/bioanuai.
Awali
Waziri Zungu amewatunuku vyeti Wakaguzi wa Mazingira 22 kutoka Wilaya za Mkoa
wa Dodoma ambao walishiriki mafunzo yalitolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
pamoja na Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC.
Siku ya
Mazingira Duniani huadhimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka. Kaulimbiu yam waka huu
ni ”Tutunze
Mazingira: Tukabiliane na Mabadiliko ya Tabianchi”.
0 comments:
Post a Comment