Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo Ndugu Gerald M. Kusaya
anawatangazia wanachuo na wakufunzi kuwa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo (MATI)
vimefunguliwa rasmi tarehe 01 Juni, 2020
kufuatia agizo la Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli alilotoa tarehe 21 Mei, 2020.
Wanafunzi
wote wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo nchini wanatakiwa kuendelea kuripoti vyuoni
kwa ajili ya kuendelea na masomo yao. Wizara
inawataka wanafunzi wote kuhakikisha wanakuwepo vyuoni ifikiapo tarehe 08 Juni,
2020 na itakapofika tarehe 10 Juni, 2020 Wakuu wa Vyuo vyote wachukue hatua za
kinidhamu na kitaaluma kwa wanafunzi ambao watakuwa hawajaripoti vyuoni.
Aidha, Wakuu wa Vyuo vyote vya Kilimo wanatakiwa wafanye maboresho ya kalenda
ya masomo kwa kuzingatia maagizo ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
yaliyotolewa tarehe 22 Mei, 2020
Wizara ya
Kilimo inasisitiza kuwa watumishi na wanafunzi wote vyuoni waendelee kuzingatia
kanuni zote za kujikinga na ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID -19) kama
zilivyotolewa katika mwongozo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto.
0 comments:
Post a Comment