Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiongea na waandishi wa habari akielezea kwa namna gani wanavyofanikiwa kutunza mazingira.
Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita akiongea na waandishi wa habari akielezea kwa namna gani wanavyofanikiwa kutunza mazingira.
NA FREDY
MGUNDA, IRINGA
ZAIDI ya
miche ya miti milioni moja hugawiwa kwa wadau na wananchi mbalimbali wa wilaya
ya Mufindi kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya misitu na wakala wa
huduma za misitu Tanzania TFS kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema
lengo la kutoa miche hiyo kuendelea kuchukua hatua madhubuti za ulinzi
shirikishi wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuondosha hatari zitokanazo
na uharibifu wa mazingira
Alisema kuwa
Jamii Taasisi mbalimbali na mashirika ya Umma
yamesisitizwa kuendelea kuthamini na kutunza mazingira kutokana na umuhimu wake
kwenye maisha ya binadamu.
Alisema ni jukumu la kila
mmoja kuendelea kuyatunza mazingira na hasa juu ya ulinzi wa Bayoanuai zilizopo
ambazo zimekuwa na manufaa makubwa kwa viumbe hai wote wakiwamo Binaadam huku
akitaja za kutoweka kwa bayoanuai
Mwita alieleza namna
ambavyo Shamba la Miti Sao Hill linavyohamasisha jamii kuendelea kuyatunza
mazingira kwa kuihusisha katika shughuli rafiki za uhifadhi wa masitu ikiwamo
ajira na ufugaji wa nyuki.
Alisema kuwa misiti imekuwa
na faida mbalimbali kwa viumbe vyote duniani ikiwepo kuwa makazi ya
wadudu,wanyama,ndege na eneo sahihi kujipatia chakula,ikolojia ya misitu ya Sao
Hill imechangia sana upatikanaji wa maji ya mto Ruaha Mkuu na Ruaha Mdogo
ambavyo hupeleka maji katika vituo vya kuzalishia umeme.
“Umeme unazalishwa katika
vituo vya Mtera,Kihansi na mwalimu Nyerere wanategemea maji kutoka katoka
hidhafi ya misitu ya Sao Hill kutokana na utunzaji bora wa ikolojia yake”alisema
Alisema upandaji wa miti
unasaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali za asili ambazo zimekuwa zinasaidia
katika maisha ya binadam hivyo misiti inaumuhimu mkubwa sana kwa wananchi kote
ulimwenguni.
Aidha Mwita alisema kuwa
shamba la miti la Sao Hill limekuwa lanachangia kukuza uchumi katika sekta
mbalimbali kama viwanda,miundombinu na sekta ya ujenzi.
Kwa upande mdau wa
mazingira kutoka Shamba la Miti Sao hill Alex Kalinga alisema kuwa wamekuwa
wananufaika na uwepo wa miti pamoja na kupewa elimu ya uhifadhi wa miti.
Nao wadau wa mazingira
kutoka Shamba la Miti Sao hill wameeleza namna wanavyonukaika na uwepo wa
shamba hilo la Serikali huku wakipongeza hatua zinazochukuliwa hasa juu ya
ulinzi wa mazingira.
meneja wa Kampuni ya uzalishaji na usafirisha wa magogo na nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprises Ntibwa Mjema wamesema
utunzaji wa mazingira ni matokeo chanya ya ukuaji wa uchumi wa wilaya ya
Mufindi na watu wake.
“kuchukua hatua za ulinzi
wa misitu na uhifadhi wa mazingira ili kuendelea kunufaika na rasilimali
zitokanazo na uhifadhi” Alisema Mjema
Siku ya Mazingira Duniani
ni siku inayotambulika zaidi ya kushughulikia mazingira. Tangu mwaka wa 1974,
imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni; ikileta pamoja
serikali, mashirika ya biashara, watu maarufu na wananchi kushughulikia masuala
nyeti ya mazingira.
0 comments:
Post a Comment