Meneja wa kampuni inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd, Ntibwa Mjema akiongea na waandishi wa habari katika kiwanda cha uzalishaji wa nguzo za umeme
Mhasibu wa kampuni inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd Abeid Mhongole akiongea na waandishi wa habari katika kiwanda cha uzalishaji wa nguzo za umeme
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
KAMPUNI inayozalisha
nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd imepongeza juhudi za kutunza mazingira
zinazofanywa na shamba la miti la Sao Hill kwa kuendelea kutoa elimu ya
upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi
wa habari Meneja wa Qwihaya, Ntibwa Mjema alisema kuwa kampuni hiyo
inawapongeza na kuwashukuru wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS
kupitia shamba la miti la Sao hill Mkoani Iringa kuwa karibu na wadau wa
misiti.
Mjema alisema kupitia shamba la
miti la Sao Hill wamefanikiwa kutoa ajira kwa wafanyakazi zaidi ya mia mbili
kupitia kiwanda hicho cha kuzalisha nguzo za Umeme ambazo kwa sasa zinasambazwa
karibia nchi nzima.
Alisema shamba la miti Sao Hill
limekuwa mfano kwa nchi nyingi Africa na nje ya Afrika kwa namna ambavyo
linatumika katika kuhifadhi mazingira na kutoa ajira kwa watanzania wengi ambao
wanapata faida kupitia shamba hilo.
Mjema alisema kuwa kupitia
mazao msitu yanayopatikana katika shamba hilo la Sao Hill wamefanikiwa
kuendeleza kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla kwa wananchi wengi hapa nchini
na nje ya nchi.
Alisema kampuni
inayozalisha nguzo za umeme ya Qwihaya General Enterprise Co Ltd inampongeza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuziamini
kampuni za wazawa katika kufanya miradi mingi ya kimaendeleo ambayo sasa
imeleta mabariko makubwa kwenye sekta mbalimbali
“Kamapuni ya Qwihaya ni
kampuni ya kizalendo ambayo imeaminiwa kuzalisha nguzo za umeme ambazo zimekuwa
zinasambazo nchi nzima hasa kwenye mradi wa REA ambao umekuwa unawanufaisha
wananchi wengi wa kijijini ambao hapo awali walikuwa hawana umeme” alisema
Aidha Mjema aliwataka
wakulima wa miti kuacha tabia ya kuvuna miti ikiwa bado michanga kwa kuwa soko
lake linakuwa halina faida kwao na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.
Kwa upande wake mhasibu
wa kampuni ya Qwihaya Abeid Mhongole alisema kampuni hiyo imeajiri wafanyakazi
zaidi ya mia mbili kutokana na mazao ya misitu ambayo yamekuwa yanatumika
kutoka katika shamba la miti la Sao Hill.
Alisema kuwa shamba la
Sao Hill limekuwa msaada mkubwa kwa kutoa ajira nyingi kwa watanzania na
kusaidia kukuza uchumi kwenye sekta ya viwanda kutokana na mazao ya misitu
ambayo yanapatikana katika shamba hilo.
Mhongole alimpongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa
anayoifanya kuleta maendeleo kwa watanzania hasa katika kuwaamini watanzania
katika kuweka kwenye miradi mikubwa ya kimaendeleo.
0 comments:
Post a Comment