Askofu Michael Msonganzila Jimbo
Katoliki Musoma akiongoza ibada ya kumshuruku mungu kwa kulisaidia taifa
kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi
vya Corona kama ilivyotabiriwa na mataifa ya nje katika Parokia ya
Shirati, ambapo alisisitiza watanzania
kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili azidi kukua na kuongezeka imani na busara katika kuliongoza taifa, jana
Wilayani Shirati,Mkoani Mara.
Baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Shirati wakifuatilia ibada ya
kumshukuru mungu kwa kuliepusha taifa na maambukizi na vifo vingi vya virusi vya Corona kama
ilivyotabiriwa na mataifa ya nje iliyokuwa ikiongoza na Askofu Michael
Msonganzila Jimbo Katoliki Musoma
(hayupo pichani) jana.
Baadhi ya viongozi wa serikali ya wilaya ya Shirati na Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika
picha ya pamoja na Askofu Michael Msonganzila
Jimbo Katoliki Musoma mara baada ya ibada ya kumshuruku mungu kwa
kulisaidia taifa kutokupata vifo vingi vya kutokana na virusi vya Corona kama ilivyotabiriwa na
mataifa ya nje, jana katika Parokia ya Shirati, mwenye tisheti ya mistari ni
Mkuu wa Wilaya ya Shirati Saimo Chacha,wa pili kushoto kwa waliyosimama mbele
ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt. Emmanuel
Temu kuto Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo.
Watanzania
tuendelea kumwombea Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe
Magufuli ili aendelee kukua na kuongezeka imani na busara.
Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma
ametoa wito huo hivi karibuni katika ibada maalum ya kumshukuru mungu
iliyofanyika katika Parokia ya Shirati kwa ajili ya kumshukuru mungu kwa
kulisaidia taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona tofauti na
ilivyotabiriwa na mataifa ya nje nah ii ni kufutia maono Mheshimiwa Rais yaliyosaidia
taifa kukabiliana na janga la maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Kwanini tung'ang'ane kupata taarifa za
idadi za vifo, taarifa hizi hazisaidii sana bali zinaongeza hofu tu
na pia hata taarifa za kweli zinapotolewa baadhi ya watu wanabeza kwa
Musoma hii mpaka sasa tunakifo kimoja tu cha mgonjwa wa Corona hakuna taarifa
zinazofichwa Kanisa Katolikili lina mfumo wa kupata taarifa kuanzia ngazi ya
familia na tunafuatilia ," alisema Askofu Msonganzila.
Pamoja na
hayo askofu huyo alieleza kuwa anafahamu katika kumshukuru mungu makundi
mbalimbali ya imani tofauti yalifanya maombi yao na katika Wilaya ya Shirati
anafahamu kuwa wapo wazee wa kijadi katika eneo hilo nao walifanya tambiko.
Halikadhalika
nae askofu huyo aliendeleea kusisitiza kuwa pamoja na idadi ya maambukizi
kupungua lakini ni vyema wananchi wanaendelea kuzingatia ushauri wa wataalamu
wa afya wa kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kuepuka
msongamano.
Kwa upande
wa Chifu wa Rorya Ngoje Ogati alisema kuwa tangu janga hilo la virusi vya
Corona lilipotangazwa wazee wa eneo hilo
kutoka koo mbalimbali walifanya tambiko la kuzuia ugonjwa huo usifike
katika eneo lao na mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja katika eneo hilo amepata
virusi hivyo.
"Katika
ibada yetu ya tambiko tuliyofanya hivi karibuni nilakuzuia maambukizi ya virusi
vya Corona katika nchi yote kwa ujumla pamoja na kushukuru kwa eneo la Rorya
kutokupata maambukizi kabisa "alisema Chifu Ogati.
Nae
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Dkt.Emmanuel Temu alishukuru uongozi wa Wilaya ya Rorya kwa kuruhusu
makundi yote ya kiimani ikiwemo la wazee wa jadi kufanya ibada ya kushukuru na
kuliombea taifa.
Halikadhalika
nae mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Rorya kutoka Kijiji cha Buturi Bi. Hudo Odemba
alisema katika eneo lao hawajawahi kupata maambukizi ya virusi vya Corona na
anaamini kuwa matambiko yaliyofanywa na wazee wa eneo hilo yamesaidia kuwakinga
pamoja na taadhari wanazochukua za kunawa mikono kwa maji tiririka kila mara.
0 comments:
Post a Comment