METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, June 1, 2020

DKT MABULA: VIONGOZI TUWE MSTARI WA MBELE KUYASEMA MAZURI YA RAIS JPM



Viongozi wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuyasema mazuri yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli kwa wananchi wao.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na  makatibu wa chama Cha mapinduzi ngazi ya matawi na kata katika ukumbi wa chuo Cha Maliasili Pasiansi ikiwa ni hitimisho la ziara yake ya kuzitembelea halmashauri kuu zote za kata  ndani ya Jimbo hilo kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi, kupokea ushauri na pongezi juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo amewataka watendaji hao kuwa mstari wa mbele katika kufafanua kwa wananchi shughuli za kimaendeleo  zinazotekelezwa na Serikali yao pamoja na kumpongeza Rais Magufuli kwa jitihada alizozichukua katika kipindi kigumu cha Janga la ugonjwa wa Covid-19 unaoenezwa na kirusi Cha Corona

'.. Bila Rais mcha Mungu, Bila Rais mwenye hofu na Mungu sijui nchi hii ingekuwa wapi?, Sasa nyinyi watendaji mnaowajibu wa kuwaelimisha wananchi wetu juu ya haya mazuri yanayofanyika..' Alisema

Aidha Mhe Dkt Mabula amempongeza Rais Magufuli kwa kuruhusu wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku badala ya kuwafungia kama zilivyofanya nchi nyingine huku akikemea baadhi ya viongozi kuhujumu utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali au viongozi katika maeneo ya Jimbo hilo jambo linalosababisha wananchi waichukie Serikali yao na Viongozi wake.


Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula amemsifu Mbunge huyo kwa jitihada zake katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku akiwataka viongozi hao kwa nafasi zao kila mmoja katika eneo lake kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhamasisha ushiriki wa wananchi kama ilivyofanya halmashauri kuu na Kamati ya siasa ya wilaya hiyo kwa kutembelea na kuridhishwa na miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ikiwemo Tanki kubwa la Maji lililopo kata ya Nyasaka, Stendi ya mabasi ya kisasa iliyopo Nyamhongolo, Barabara ya kutoka Nyakato-Buswelu, Barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu na Ujenzi wa kituo Cha afya Buzuruga.

Nae katibu wa CCM tawi la Bwiru Press Ndugu Johnson Mahuba kwa niaba ya makatibu wengine akamshukuru Mbunge huyo kwa jitihada zake katika kutatua migogoro ya ardhi iliyokuwa ikiwakabili wananchi hao hasa ule wa eneo la Bwiru anakoishi sanjari na kuipongeza manispaa ya Ilemela kwa namna inavyojitahidi katika kuendesha zoezi la upimaji shirikishi.

Kupitia kikao hicho Mbunge Dkt Angeline Mabula akakabidhi Shajara na vifaa vya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwa makatibu wa kata na matawi ili kurahisisha utekelezaji wa shughuli zao za kila siku vikiwemo ndoo za maji 130, vitakasa mikono 130, kalamu box 20, counter book 150, ream paper katoni 33, na sabuni za kunawia mikono katoni 150 vyote vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 8 na laki 5.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com