Kampuni ya Kimataifa ya Magari ya TATA Africa Holding Ltd imemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda Gari Moja kati ya mbili walizoahidi kumpatia kama sehemu ya Mchango katika mapambano dhidi ya Corona katika Mkoa huo.
Gari hiyo aina ya XENON X2 Double Cabin RC Makonda ameelekeza itumike kuwasafirisha Watumishi wa Afya wanaofanya kazi ya Mapambano dhidi ya Corona.
Aidha RC Makonda ameishukuru kampuni hiyo kwa mchango walioutoa na kusema Gari hiyo itaenda kutatua changamoto za usafiri zilizokuwa zikiwakabili watumishi wa Sekta ya Afya huku akieleza kuwa hali ya Maambukizi ya Corona katika Mkoa huo imepungua na Wagonjwa wengi wanazidi kupona.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya TATA Motors, Bwana Rajiv Bhushan amesema kwa siku ya leo wamekabidhi Gari moja ambapo Gari ya pili wataikabidhi muda wowote kuanzia sasa.
Aidha Bw.Rajiv amesema Kampuni hiyo imeona ni vyema ikawa sehemu ya mchango kwa jamii katika mapambano dhidi ya Corona kwa kuhakikisha watoa huduma wa Afya wanakuwa na usafiri wa uhakika.
0 comments:
Post a Comment