Waziri wa
Nishari, Dkt. Medard Kalemani( kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin
Shigela( kulia) wakiteta jambo baada ya waziri wa nishati, kufanya ziara katika
ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta Kampuni ya GBP mkoani Tanga, Mei 10, 2020.
Kamishna wa
Maendeleo Petroli wa Wizara ya Nishati, Adam Zuber( kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa pamoja nchini( PBPA) erasto
samwel( katikati) walimsikiliza Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani,(
hayupo pichani) akizungumza baada ya kufanya ziara katika ghala ya kuhifadhi na
Kupokea mafuta Kampuni ya GBP mkoani Tanga, Mei 10,2020.
Waziri wa
Nishari, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia)akipita kukagua mazingira ya ghala
la kuhifadhi na kupokea mafuta la kampuni ya GBP, alipofanya ziara katika eneo
hilo mkoani Tanga, Mei 10, 2020.
Shehena ya
Mafuta ikiwa imepakiwa katika matangi tayari kwa kusafirishwa,hapa ni katika
ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta la kampuni ya GBP mkoani Tanga, Waziri wa
Nishari, Dkt. Medard Kalemani, alifanya ziara katika eneo hilo, Mei 10,2020.
Baadhi ya
mapipa makubwa ya kuhifadhia mafuta katika ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta
la kampuni ya GBP mkoani Tanga, Waziri wa Nishari, Dkt. Medard Kalemani,
alifanya ziara katika eneo hilo, Mei 10, 2020.
Waziri wa
Nishati, Dkt Medard Kalemani, ametoa siku kumi kwa Mamlaka ya Udhibiti huduma
za Nishati na Maji (EWURA) kumpatia majibu ya uwiano wa viwango vya bei ya
mafuta katika maghala ya Kupokea na kuhifadhia mafuta nchini.
Dkt.
Kalemani alisema hayo alipofanya ziara ya kutembelea ghala la kuhifadhia mafuta
la kampuni ya GBP iliyoko mkoani Tanga, Mei 10, 2020, ili kuona kama agizo lake
alilolitoa mwezi Machi, 2020, la kuwataka waagizaji mafuta nchini wanaagiza
shehena kubwa kutokana na tishio la kuwepo kwa virusi vya Corona.
Pia
alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini katika
wilaya ya Mkinga na Muheza mkoani huo pamoja na kuwasha umeme.
Baada ya kupata
taarifa ya mwenendo wa uingizaji,upokeaji na uhifadhi wa mafuta nchini katika
maghala pamoja na mambo mengine, Dkt.Kalemani aliiagiza EWURA kufanya tathmini
ya bei ya mafuta katika maghala hayo kwa lengo la kuboresha biashara ya mafuta
kwa maslahi ya watumiaji na wafanyabiashara.
Dkt.Kalimani
alisema kuwa, serikali imeweka utaratibu wa kuweka maghala ya kupokea na
kuhifadhi mafuta katika kila ukanda wa nchi kwa lengo la kuwapunguzia gharama
za usafiri wafanyabiashara wa mafuta wanaotembea umbali mrefu kuyafuata mafuta
hayo, pia kuwezesha watumiaji kupata huduma hiyo kwa haraka, karibu na kwa bei
nafuu wakati wote.
Sambamba na
hilo kulinda ubora wa miundombinu ya barabara nchini kwa kuwa magari yanayobeba
mizigo mizito ikiwemo mafuta yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa uharibifu
wa barabara.
“EWURA na
PBPA nawapa siku 10,muangalieni uwiano na uratibu sahihi wa bei ya mafuta
katika maghala ili bei hizo zisitofautiane sana na taratibu za bei zilizowekwa,
kwa kuwa mafuta yapo mengi nayakutosha, na mniletee majibu, Lengo la serikali
ni kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa urahisi na kwa bei nafuu wakati wote kwa
kuwanufaisha wafanyabiashara na watumiaji”, alisema Dkt. Kalemani.
Alitoa wito
kwa wafanyabiashara wa mafuta kwa kanda ya kaskazini ikiwemo Mikoa ya Arusha,
Kilimanjaro,Manyara na Tanga kutumia ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta
lililopo mkoani Tanga kuliko kuyafuata mkoani Dar Es Salaam.
“Wafanyabiashara
wanaofuata mafuta Dar es salam watalazimika kuuza kuwauzia watumiaji kwa bei ya
juu hivyo kuwakandamiza watumiaji hii si sahihi na ndiyo maana karibu kila
ukanda wa nchi tumeweka ghala la kuhifadhi na kupokea mafuta,tofauti na
ilivyokuwa awali mafuta yote yalikuwa yakipatikana mkoani Dar Es Salaam
pekee”,alisisitiza Dkt. Kalemani
Alitoa wito
kwa makampuni yote ya uwagizaji wa mafuta nchini kwa kushirikiana na EWURA na
Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa pamoja (PBPA)kushirikiana kwa pamoja kuendelea
kuleta mafuta mara dufu ili kujihakikishia uwepo wa mafuta nchini hata kama
ugonjwa wa corona utaendelea kuwepo.
Dkt.
Kalemani alifafanua kuwa mafuta yaliyopo nchini kwa sasa yanauwezo wa kutumika
zaidi ya miezi miwili hadi mitatu mbele na bado kila siku wanapokea mafuta,
ambapo kwa sasa nchi inapokea inapokea mafuta lita milioni 428.7 tofauti na
awali kabla ya agizo kutoka ilikuwa ikipokea mafuta lita milioni 185.
Aidha
aliwataka wafanyabiashara ya mafuta kujenga vituo vya mafuta katika maeneo
yaliyo vijijini ili kulinda ubora wa mafuta na kusogeza huduma karibu na
watumiaji hasa wadogo akitolea mfano waendesha pikipiki ambao ndiyo
wanaotegemeo kubwa la usafiri katika maeneo ya vijijini.
Alisema
kuwa watumiaji wadogo wa vyombo vya moto, wamekuwa wakisafiri umbali mrefu
kutafuta huduma ya mafuta, na wengine wamekuwa wakihifadhi mafuta katika nyumba
zao jambo ambalo linahatarisha usalama wao.
Aidha
alisema kuwa pia kumekuwa na tabia ya kuuza kiholela mafuta na uhifadhi mbovu
wa mafuta hayo na hivyo kupunuza ubora waviwango vya mafuata kwa watumiaji na
hivyo hata kulazimu mafuta hayo kuchanganywa na hivyo kuchangi uharibifu wa
yyombo vinavyotumia mafuta hayo.
“Wafanyabiashara
nendeni mkajenge vituo vidogo vya mafuta vijijini, mrahisishe huduma ya
upatikanaji wa mafuta na bei nafuu kwa watumiaji wadogo ambao wamekuwa
wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo,tuungane kutekeleza lengo la
serikali la kuhakikisha kila mtumiaji wa mafuta anapata bishaa hiyo kwa wakati
na kwa bei nafuu”, alisisitiza Dkt. Kalemani.
Pamoja na
mambo mengine alitembelea eneo inapojengwa kifaa kitakachotumika kupima mafuta
(Flow Meter), yanayoingia nchini kutoka katika Meli kwenda katika maghala ya
kuhifadhi na kupokea mafuta katika
Bandari ya Tanga.
Aliiagiza
mamlaka ya bandari nchini kukamilisha ujenzi wa mtambo huo haraka ili serikali
ipate kiwango sahihi cha mafuta yanayoingia nchini kupitia Bandari ya Tanga ili
kupata kodi na tozo stahiki.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uagizaji mafuta ya GBP, Badar Seif Sood
alimueleza Waziri wa Nishati kuwa wamefanya upanuzi wa bandari hiyo, hivyo kwa
sasa inauwezo wa kuhifadhi na kupokea mafuta lita milioni 182, tofauti na
walivyokuwa wananza mwaka 2017 walipokuwa wakihifadhi na kupokea mafuta lita
milioni 182, na upanuzi utaendelea kulingana na mahitaji.
Aliishukuru
serikali kupitia wizara ya nishati, kuendelea kuwalinda wafanyabiashata wa
mafuta wakiwamo wamiliki wa maghala ya kuhifadhi na kupokea mafuta pamoja na
waagizaji wakubwa wa mafuta kwa kuhakikisha wanafanya biashara zao katika
mazingira rafiki: Huku akiahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa watumiaji wa
mafuta hayo nchini.
Katika
ziara hiyo, Dkt. Kalemani, pia alikagua maendeleo ya usambazaji wa umeme
vijijini katika Wilaya ya Mkinga na kuwasha umeme katika kijiji cha Mbuyuni
kata ya Mapatano na kutembelea kisima cha maji katika kijiji cha Jihirini na
kuliagiza Shirika la Umeme nchini (TANESCO), kupeleka na kuwasha umeme katika
kisima hicho mwishoni mwa mwezi huu.
Vilevile
alitembelea Wilaya ya Muheza na kukagua kazi ya usambazaji wa umeme katika
kijiji cha Kwakokwe na kuwataka wananchi kuendelea kulipia gharama za
kuunganishiwa umeme kwa kuwa vijijini vyote nchini vitapata umeme na kwamba
wasikubali kuuziwa miundombinu ya umeme na pia watumie wakadarasi
wanaotambulika na TANESCO katika kutandaza nyaya katika nyumba zao.
0 comments:
Post a Comment