Serikali inaendelea na zoezi la Kidemokrasia la
wananchi kuboresha taarifa za wananchi kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
ambazo zitatumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Mdiwani unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 2020.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi ameongoza zoezi hilo
kwa Makatibu Wakuu leo Mei 04, 2020 hapa jijini Dodoma kuhakiki na kuhuisha
taarifa zao katika ikizingatiwa leo ni siku ya mwisho kwa zoezi hilo nchini kote.
“Serikali inaendelea kukamilisha kuboresha
Daftari la Kudumu la Mpiga Kura, Serikali zoezi hili ni muhimu sana kwa nchi
yetu ikizingatiwa ni la kidemokrasia licha ya kwamba nchi yetu na dunia nzima
inapitia kwenye changamoto tuliyonayo ya COVID-19” alisema Dkt. Abbasi.
Ameongeza kuwa Demokrasia itaendelea
kuheshimiwa nchini kwa sababu ni kitu muhimu sana na viongozi hao pamoja na
wananchi waliojiandikisha kutumia haki yao ya Kikatiba kuchagua viongozi wao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba
na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema kuwa Wizara yake inajukumu la kuhamasisha
mambo mbalimbali ikiwemo elimu ya haki ya Mpiga kura.
“Nchi yetu imepiga hatua kubwa sana katika
demokrasia kiasi kwamba tunajivunia hatua tuliyofika ni nzuri na demokrasia imekuwa
ni ya kweli hakuna mwaka ambao tumevuka miaka mitano hatujafanya uchaguzi na
wanannchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wao” alisema
Prof. Mchome.
Lengo la elimu ya mpiga kura ni kuwahamasisha
wananchi kutumia haki yao ya kikatiba katika kujitokeza na kushiriki kuchagua
viongozi wao watakao waongoza ili kujenga Demokrasia na Utawala Bora nchini
hatua inaanza kwa wananachi kijiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Mpiga
Kura ambalo linaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
0 comments:
Post a Comment