Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi
wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Qwihaya General Enterpises Co. Limited,
Leonard Mahenda, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za
Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma, Mai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya
Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha
nguzo ya Mufindi Woodpoles Plant and Timber Limited, Salim Ahmed Abeid, ikiwa
ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya
ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza
baada ya kupokea hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/=, zikiwa ni
mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya
ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika
kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye
thamani ya Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono
juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID -
19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama
amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani ya sh. milioni 150 zilizotolewa na
kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme nchini kwa ajili ya kusaidia
mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona
(COVID- 19).
Waziri amepokea michango hiyo kwa niaba ya
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 4 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri
Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo imetolewa na kampuni Mufindi
Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General Enterprises Co Ltd na Poles (T)
Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.
Akizungumza wakati wa kupokea michango hiyo
Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa kuunga mkono jitihada
za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.
“Nawashukuru sana kwa niaba ya Serikali na hii
inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa ni sehemu ya
mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri Mhagama.
Pia, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo
kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na Watanzania kuendelea kushirikiana na
Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali ili kuwezesha katika kukabiliana na
janga hilo.
“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu
na kuguswa na janga hili kwa kuchangia kwa kadiri inavyofaa ili kuendeleza uzalendo
kwa hali ya kujali na kuonesha utayari ili kudumisha hali ya utamaduni uliopo
tangu awali wa umoja na mshikamano ,”alisema Waziri Mhagama.
Aliwahakikishia wadau hao kuwa, michango hiyo
itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa imefika katika eneo
salama.
Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani
aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa michanga waliyoitoa kwa Serikali
ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.
“Niwapongeze wakandarasi hawa kwa kuonesha nia
ya kushiriki katika mapambano haya na wito wangu kila anayeguswa na janga hili
ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini katika kuhudumia na kusaidia katika
kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi wengine waige, ”alisema Dkt. Kalemani.
0 comments:
Post a Comment