Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza amesema msaada huo umelenga kuwawezesha watoto hao kusherehekea vyema sikukuu ya Eid El Hajj / Eid ya kuchinja
Sheikh Luseza amesema kwa kawaida sherehe za Idd el Hajj /Eid El Adh-ha kwa waumini wa kiislamu huambatana na sunna ya kuchinja wanyama ikiwa ni katika kukumbuka tukio kubwa la Nabii Ibrahim (AS) aliyeagizwa na mwenyezi mungu amtoe sadaka mwanaye wa kiume Ismael.
Sheikh Luseza mesema kutokana na hali hiyo kila mwaka waislamu wote ulimwenguni huadhimisha sherehe za Idd el Hajj ambazo huambatana na ibada ya kutekeleza nguzo ya tano ya kwenda kuhiji katika mji mtukufu wa Makka kwa waumini wenye uwezo wa kwenda huko.
Amesema hitimisho la ibada ya kuhiji huambatana na sunna ya kuchinja wanyama ambapo pia waislamu wengine ambao hawakupata uwezo wa kwenda kuhiji hutekeleza ibada hiyo kwa kufunga na kuchinja wanyama ambao hutolewa sadaka kwa watu mbalimbali.
Nao Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija, Seleman Kipanya na Ustadh Ally Salim Ally kutoka kituo kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans (SORC,wameushukuru uongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya kwa kuwakumbuka watoto wanaolelewa katika kituo chake na kwamba msaada walioutoa utawezesha pia kuungana na waislamu wengine katika kusherehekea Idd el Hajj.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama
Malunde ametusogezea picha 16 kutoka katika kituo walemavu wa ngozi
(Albino) cha Buhangija na kituo cha watoto yatima cha Shinyanga Society
for Orphans (SORC)

Watoto katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga wakiangalia zawadi ya mbuzi wawili na mchele kilo 50 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Hajj

Zoezi la kushusha mbuzi kutoka kwenye gari likiendelea..Kulia aliyevaa suti ni kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza ,kulia kwake ni msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Selemani Kipanya
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza (mwenye suti nyeusi) akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya
mbuzi wawili na mchele
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa watoto wenye
albinism,wasioona na wasiosikia katika kituo cha Buhangija
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya sikukuu ya Eid El Hajj
ambapo alisema Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya itaendelea kutembelea
kituo hicho na vituo vingine na kutoa msaada kadri itakavyowezekana.

Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akimshukuru Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza kwa kuwapatia zawadi ya sikukuu ya Eid El Hajj
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akiteta jambo na mmoja wa watoto katika kituo cha Buhangija
Masudi Salum baada ya kukabidhi zawadi

Watoto katika kituo hicho baada ya kupokea zawadi hiyo

Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans (SORC) chenye jumla ya watoto 60 kilichopo katika manispaa ya Shinyanga ambapo pia Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga imetoa zawadi ya mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Hajj
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akiwa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga
Society for Orphans (SORC)
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akisalimiana na watoto katika kituo cha kulelea watoto yatima cha
Shinyanga Society for Orphans (SORC)

Luseza akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi ya mbuzi wawili katika
kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans (SORC)
Kiongozi
wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani
Luseza akishikana mkono na mmoja wa walimu katika kituo cha Shinyanga
Society for Orphans (SORC, Ustadh Ally Salim Ally wakati wa kukabidhi
zawadi ya sikukuu ya Eid El Hajj

Katikati ni Ustadh Ally Salim Ally akishukuru baada ya kupokea zawadi ya mbuzi wawili kwa ajili ya watoto wa kituo hicho

Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza akiteta jambo na Ustadhi Ally Salim Ally-Picha zote na Kadama Malunde
Watoto katika kituo cha walemavu wa ngozi cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga wakiangalia zawadi ya mbuzi wawili na mchele kilo 50 kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Hajj
Zoezi la kushusha mbuzi kutoka kwenye gari likiendelea..Kulia aliyevaa suti ni kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza ,kulia kwake ni msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Selemani Kipanya
Msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Seleman Kipanya akimshukuru Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza kwa kuwapatia zawadi ya sikukuu ya Eid El Hajj
Watoto katika kituo hicho baada ya kupokea zawadi hiyo
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Shinyanga Society for Orphans (SORC) chenye jumla ya watoto 60 kilichopo katika manispaa ya Shinyanga ambapo pia Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga imetoa zawadi ya mbuzi kwa ajili ya sikukuu ya Eid El Hajj
Katikati ni Ustadh Ally Salim Ally akishukuru baada ya kupokea zawadi ya mbuzi wawili kwa ajili ya watoto wa kituo hicho
Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya mkoani Shinyanga, Sheikh Shabani Luseza akiteta jambo na Ustadhi Ally Salim Ally-Picha zote na Kadama Malunde
0 comments:
Post a Comment