Kamanda wa kitengo cha Usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango pichani.(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi
Kikosi
cha usalama barabarani mkoa wa Pwani kimeliingizia serikali mapato ya
zaidi ya sh.bil.2.033 katika kipindi cha januari hadi agosti mwaka huu .
Kikosi hicho kimekusanya mapato hayo kupitia ukamataji wa makosa mbalimbali ya usalama barabarani mkoani humo.
Mkuu wa
usalama barabarani mkoani Pwani, Abdi Issango alisema katika kupambana
na ajali wameweza kuendesha misako na kufanya ukaguzi mbalimbali katika
barabara kuu na za ndani ya miji.
Alieleza
kuwa kwa kipindi miezi nane wamekamata jumla ya makosa 68,109 ambapo
yaliyolipiwa kiasi hicho cha fedha ni 67,785 mwaka huu.
Kamanda
Issango alisema makosa hayo yakilinganishwa na ya mwaka jana kipindi
hicho kuna ongezeko la makosa 20,797 ambayo ni sawa na ongezeko la sh.
mil. 569,400 sawa na asilimia 38.89.
Alisema
kuwa katika kipindi kama hicho mwaka 2015 kitengo hicho kilikamata
makosa 47,109 na yaliyolipiwa ni 46,988 sh.bil. 1,464,150.
Aidha
akizungumzia matumizi ya speed radar mpya 24 za kisasa walizopewa mwaka
jana ambazo zinapiga picha na kurekodi wameweza kukamata makosa ya
magari yanayokwenda kwa mwendo kasi 32,753 .
Kamanda
Issango alisema magari hayo yaliyokamatwa kwa ajili ya kukimbiza magari
yalilipiwa faini sh. mil 982,590 kutoka januari hadi agosti mwaka huu.
“Vitendea
kazi tulivyonavyo ikiwa ni pamoja na speed radar hizi za kisasa,
tunaweza kusema sisi Pwani tumefanikiwa kudhibiti ajali zitokanazo na
mwendo kasi kwa asilimia 100 hasa mabasi ya abiria”alisema Issango.
Hata
hivyo kitengo hicho kuelekea maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
barabarani wameanza kutoa mafunzo mbalimbali kwa waendesha
pikipiki,wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na mikusanyiko ya
watu ili kuwapa uelewa wa matumizi sahihi ya alama za barabarani.
0 comments:
Post a Comment