Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada kwa ajili ya wahanga wa kitongoji cha Mbingama tarafa ya Pawaga.
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
MJUMBE wa mkutano mkuu wa CCM
Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri ametoa msaada wa chakula
tani tatu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wa kijiji cha
Isele kilichoko tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoanbi
Iringa kwa kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya chakula.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, Arifu Abri alisema
kuwa changamoto wanayokabiliana nayo
wananchi wa kijiji hicho imepelekea kujitoa kuwasaidia watu wenye mahitaji
muhimu ili kuokoa maisha yao madhara waliyopata kutokana na mafuriko hayo.
Alisema alipata taarifa ya
wananchi wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele kuwa wamepatwa na mafuriko
kutokana na kunyesha kwa mvua nyingi msimu huu wa kilimo na kusabaisha hasara
kubwa kwa wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo lililotokea mafuriko na
kutegemea zaidi kilimo kwa ajili ya maisha.
Alisema kuwa moja ya mahitaji
ambayo wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama ni wananchi asilimia kubwa
kukosa chakula cha kila siku hivyo ndio maana msaada wangu nimejielekeza kwenye
kutoa chakula zaidi ambapo utawasaidia kwa kipindi hiki cha mafuriko.
“Najua kuna wadau wengine
wameshatoa baadhi ya msaada kulingana na mahitaji hata hivyo kwa upande wangu
mimi nimeamua kutoa chakula kulingana na mahitaji ambayo nimeona wanahitaji
wahanga wa mafuriko wa kitongoji cha Mbingama kijiji cha Isele Tarafa ya Pawaga”
alisema
Abri alitoa wito kwa wadau
wengine kuendelea kujitokeza kuwasaidia wahanga hao wa mafuriko katika
kitongoji cha Mbingama ili kuwasaidia kurudi kwenye maisha ambayo walikuwa
wameyazoe hapo awali kulingana na shughuli ambazo walikuwa wanazifanya kupa riziki
zao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya
ya Iringa, Richard Kasesela mara baada ya kupokea msaada huo alimshukuru mjumbe
wa mkutano mkuu ccm taifaArifu kwa msaada huo kwa kuwa umekuja katika wakati
mwafaka kutokana na changamoto wanazokabiliana nazo wananchi hao.
Aidha Kasesela alitoa wito kwa
wadau kujitokeza zaidi kuwasaidia wananchi hao ambao licha ya changamoto ya
chakula wanakabiliwa na changamoto ya nguo, makazi, madawa kwa lengo la kuweza
kuondokana na hali hiyo.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana Wilaya ya Iringa Makala Mapesah alisema kuwa wadau kama arifu Abri
wanatakiwa kuigwa katika jamii zetu kwa watu wenye uwezo kuwasidia watu ambao
wanakuwa wanamahitaji ili waendelee kuishi kama wananchi wengine wanaopata
mahitaji mengine.
“Mimi kama mwenyekiti niwaombe
wadau wengine waendelee kujitolea kama mdau huyu Arifu Abri ambaye amekuwa
msaada sana kwa wananchi wa wilaya ya Iringa vijijini kuwasiadia wananchi
mbalimbali hivyo lazima nimpongeze sana kwa kazi yake” alisema Makala
Katibu wa mbunge wa jimbo la
Isimani Thom Malenga alisema wahanga wa mafuriko ya kitongoji cha Mbingama bado
wanahitaji msaada zaidi hivyo anampongeza mdau Arifu Abri na kuwaomba wadau
wengine kujitokeza kutoa msaada kwa wahanga hao.
0 comments:
Post a Comment