Kushoto ni katibu wa mbunge wa Jimbo la Isimani Thom Malenga akimkabidhi ndoo maalum za kujikinga na Corona mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela zilizotolewa na Mbunge William Lukuvi kwa ajili ya wananchi wa jimbo hilo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ndoo hizo maalum kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona
mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya ya Iringa vijijini Makala Mapessah akiwaonyesha waandishi wa ha bari ndoo maalum za kujikinga na Corona zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi
NA FREDY MGUNDA, IRINGA
WAZIRI wa ardhi,nyumba na maendeleo
ya makazi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Isimani Mkoani Iringa Mh. William
Lukuvi amekabidhi kwa wananchi wa jimbo hilo jumla ya ndoo 270 maalum za kunawia mikono kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya
virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa Covid 19.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
ndoo hizo Katibu wa mbunge huyo Thom Malenga alisema kuwa vifaa hivyo
vimetolewa kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa jimbo la Isimani kutekeleza kwa
vitendo ushauri wa wizara ya afya nchini inayomtaka kila mwananchi kunawa mara
kwa mara ili kujiepusha na maambukizi ya Corona
Katibu huyo aliwahimiza
wananchi kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya na kuzitumia ndoo hizo kwa kutakasa
mikono kila wakati kwa kuwa ndio moja ya kinga ambayo inaweza kuepuka kukumbwa
na maambukizi ya virusi hivyo ambavyo vimekuwa hatari kwa maisha ya Binadam
Malenga alisema kuwa mbunge
ametoa ndoo maalumu nne kwa kila kijiji ambacho kipo katika jimbo la Isimani
kwa lengo la kusaidia katika maeneo yenye mikusanyiko na maeneo maalum kama
ofisi za kijiji,virabu vya pombe na sehemu za kuabudia.
“Leo tumekabidhi ndoo maalum
zenye uwezo wa kubeba lita Ishirini kwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela kwa lengo la kusaidia kujikinga na virusi vya Corona,kinga bora kuliko
tiba hii ndio sababu ya mbunge kutoa msaada huu” alisema Malenga
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya
Iringa Richard Kasesela alisema mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi
amekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha anawasaidia wananchi wake kwa kila jambo
linapotokea huku akiwahimiza wabunge na viongozi wengine kuiga mfano wa
kujitolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi.
“Jukumu letu ni kuhakikisha
tunawatafutia sabuni wananchi ambao hawawezi kununua ili kuwasaidia kujikinga
na virusi vya Corona” alisema Kasesela
Kasesela alisema kuwa ndoo hizo
maalum zinaghama kubwa hivyo wananchi wanapaswa kuzitunza na kuendelea kumheshimu
mbunge huyo kwa juhudi ambazo amekuwa akizitoa kuhakikisha wananchi wanapata
mahitaji muhimu kwa maendeleo.
Hadi kufikia hii leo wilaya ya
Iringa haijapata mgonjwa yeyote yule mwenye maambukizi ya virusi vya Corona
hivyo bado wananchi wapo salama na wanapaswa kuendelea kujikinga na virusi
hivyo.
Naye mwenyekiti wa umoja wa
vijana Wilaya ya Iringa vijijini Makala Mapessah alimpongeza mbunge huyo kwa
kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha wananchi wa jimbo la Isimani wanakuwa salama
kwa kujikinga na virusi vya Corona.
0 comments:
Post a Comment