Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia. Kupitia mkutano huo Tanzania imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (katikati) akiwa na baadhi ya washiriki mbalimbali wa mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara hili. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa, Beatrice Kessy
Baadhi ya Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakifuatilia mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika katika kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19 ambao umeathiri sekta ya utalii duniani kote kwa kiasi kukibwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akIfuatilia mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ulioanza kufanyika kuanzia jana tarehe 14 Juni, 2021 katika Jiji la Windhoek nchini Namibia. Kupitia mkutano huo Tanzania yatajwa kufanya vizuri katika masuala ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa COVID – 19
Baadhi ya Washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika wakifuatilia mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) wakifuatilia wasilisho la lenye lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika katika kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19 ambao umeathiri sekta ya utalii duniani kote kwa kiasi kukibwa
Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara, Beatrice Kessy kutoka Hifadhi za Taifa (TANAPA) akizungumza wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Utalii wa Kanda ya Afrika ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) ambapo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee Barabi Afrika ambapo ameomba ushirikiano wa makampuni makubwa ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Tanzania ili viweze kujulikana na watu wengi duniani ili kuongeza idadi ya watalii wataokatembelea Tanzania , Mkutano huo unaofanyika kwa muda wa siku tatu katika Jiji la Windhoek nchini Namibia.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akifanya kikao cha ana kwa ana mbobezi wa kimataifa wa kutangza vivutio vya Utalii kutoka Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii ( UNWTO) Bi. Olgo Nowak mara baada ya kufanya wasilisho lake lengo la kuzijengea uwezo nchi za Afrika kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko Afrika kupitia mitandao ya kijamii ambapo Tanzania imetajwa kung’ara kumi bora kwa nchi za Afrika kwa kutangaza vivutio vyake vya utalii kwa muda wa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2017 hadi mwaka 2020. Kushoto ni Kamishna Msaidizi Maendeleo ya Biashara kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa, Beatrice Kessy
Katika mkutano huo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ameambatana na Watalaamu wake kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wanashiriki ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi na vya kipekee ambavyo havipatikani mahali popote duniani isipokuwa Tanzania
Katika kumi bora hiyo, Afrika ya Kusini imetajwa kushika nafasi ya kwanza ikifutiwa na nchi ya Misri katika utangazaji vyema ya vivutio vyake vya utalii.
Aidha katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa kuendelea kuongoza na kufanya vizuri katika sekta ya utalii licha ya uwepo wa changamoto wa ugonjwa wa UVIKO19 ambao umeikumba karibu Mataifa mbalimbali duniani kote.
Tanzania imekuwa na vivutio mbalimbali vinavyotamba Duniani ikiwemo mlima mrefu barani Afrika, Mlima Kilimanjaro, Hifadhi zenye vivutio vikubwa vya Wanyama kama Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Nyerere, Hifadhi ya Ruaha, Tarangile,l pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro
Katika hatua nyingine Tanzania kushiriki katika mkutano huo kupitia Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na wataalamu imepata fursa ya kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa hususan viongozi wa Serikali na wadau wa utalii kutoka nchi wanachama wa UNWTO katika kukabiliana na athari za COVID-19 na kuandaa mikakati madhubuti ya kurejesha sekta ya utalii katika hali ya awali kwa kufanya vikao vya ana kwa ana na viongozi wanaoshiriki mkutano huo.
Pia, Tanzania imepata fursa ya kutoa maoni yake kwa lengo la kuimarisha utangazaji wa vivutio vya utalii vilivyopo Bara la Afrika ikizingatiwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vivutio vingi na vya kipekee katika Bara la Afrika ambapo Waziri Dkt. Ndumbaro amemkaribisha Mtaalamu wa masuala ya utangazaji kuja Tanzania kutoa ujuzi huo.
0 comments:
Post a Comment