METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, March 4, 2020

WAZIRI ZUNGU AFANYA ZIARA WILAYANI SENGEREMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akisikiliza taarifa ya msitu wa asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye ekari 12.3 kutoka kwa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Salim Ali (kulia) alipofanya ziara wilayani humo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo Joseph Kipole na wa pili kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya hiyo, Magesa Mafuru.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akiangalia msitu wa asili wa hifadhi ya miti aina ya miombo na mitundu yenye ekari 12.3 uliopomeneo la makamu makuu ya Halmashauri hya wilaya ya Sengerema ambao unatumika kama shamba darasa kwa wananchi kuhusu uhifadhi endelevu wa mkisitu yua asili katika maeneo hayo ambao kwa mujibu wa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Sengerema Salim Ali, utasaidia kunyonya hewa chafu, upatikakaji wa kuni kupitia uvunaji maalumu na uwekaji wa shughuli rafiki wa mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akipanda mti na mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani wilayani Sengerema mkoani Mwanza alipofanya ziara ambapo pia alizungumza na wanafunzi wa shule hiyo kuhusu utunzaji mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akitembelea na kukagua kikundi cha mazingira Bwawani wilayani Sengerema mkoani Mwanza ambapo aliwapongeza na kuwatangaza kuwa mabalozi wa Mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mnadani ambapo aliwataka wawe mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com