mgeni Rasmi katika kongamano la vijana Mhe. Adamu Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara akihutubia wakati wa kufunga kongamano hilo lililodumu kwa sikumbili mfululizo.
Vijana waliohudhuria kongamano la fursa katika kilimo lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Kanisa Katoliki wilani Butiama wakimsikiliza kwa makini muwezeshaji wa dawati la mikopo kutoka benki ya NMB kutoka wilaya ni Bunda
Makamu mwenyekiti wa kongamano Dkt. Zakariya Muyengi akifananua jambo wakati wa kongamano hilo.
Na Bashiri Salum, Butiama
Mkuu wa Mkoa wa Mara
Mhe. Adamu Malima amewataka vijana kujiunga katika vikundi na kuzalisha kwa
wingi matunda kwa kuwa mahitaji yake ni makubwa ndani na nje ya nchi.
Hayo ameyasema hivi
karibuni wakati wa kufunga kongamano la vijana wakulima lililofanyika kwa siku
mbili mfululizo katika ukumbi wa kanisa Katoliki Wilaya ya Butiama Mkoani humo.
Akitolea mfano
kampuni ya Bakharesa iliyopo Jijini Dar
es salaam na Jambo iliyopo mkoani Shinyanga
amesema makampuni hayo yapo tayari kuingia mkataba na wakulima wa matunda hivyo vijana wametakiwa kutumia fursa hiyo.
Mhe. Malima
ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara
ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa hatua za kubainisha fursa za kilimo mifugo na uvuvi
kwa wakulima vijana kupitia makongamano yanayoendelea kufanyika katika kanda mbalimbali hapa Nchini.
Aidha amesema kwamba
serikali ya mkoa itatoa ushirikiano mkubwa kwa vijana ikiwemo kuwapatia ardhi ya kulimo mifugo na
uvuvi ambapo kikundi na aridhi vitaendelea
kuwa mali ya Kijiji.
Katika hatua nyinge
Mhe. Malima ameliomba shirika la SUGECO (The Sokoine University Graduate
Entrepreneurs Cooperative) kuandaa utaraibu kwa kushirikiana na Hamlashauri husika
elimu ya vitendo katika Halmashauri ili
kupunguza gharama za wakulima kufuata
Kamba atamizi zilizopo mkongo wilayani
Rufiji mkoa wa pwani kwa mafunzo.
’Hapa kuna wakulima Zaidi
ya 250 kama wote wakishawishika
watatakaiwa kuwafuta SUGECO walipo ili kufanya kazi kwa vitendo kwa muda
mrefu, hili sio sawa , shirika hili liandae utaratibu kwa kushirikiana na
Halmashauri zetu wapate eneo wao ndio wawafuate wakulima’. Alisema
Mhe. Malima.
Kabla ya kufunga
kongamano hilo aliwataka vijana kushiriki ufugaji wa nyuki ambao utasaidia kutunza mazingira kwa kupanda
miti stahiki ambapo vijana hao watapata
kipato na uchumi wa taifa utakuwa Zaidi.
0 comments:
Post a Comment