Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimefurahishwa na msimamo idara uliotolewa na Waziir Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya serikali ya Rais Dkt John Magufuli , unaozitaka Nchi wanachama za SADC kusimama pamojao na Zimbabwe mpaka pale vikwazo dhalimu vya kiuchumi nchini humo zitakapoondolwa.
Kimesema wakati huu dunia nzima ikikumbwa na janga la kusambaa kwa virusi vya Corona huku huduma za kibinadamu zikihitajika kwa kiasi kikubwa haipendezi kuishuhudia zimbabwe ikiendelea kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.
Matamshi hayo yametamkwa jana na Katibu wa CCM Mkoa Morogoro Shaka Hamdu Shaka ofisini kwake akiipongeza hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa aliyotoa wakati alipofungua kikao cha mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Maendeleo ya kiuchumi Kusini mwa Afrika (sadc).
Shaka alisema vikwazo hivyo vinaapaswa kuondosha kwa hiari kwa kujali haki na kuthamini ubinadanu lakini kipindi hiki wakati dunia ikikabiliwa na mazingira ya kijografia yenye joto kali na mtafaruku, vifo na majanga, vikwazo hivyo ni manyanyaso na dhulma kwa binadamu wasio na hatua.
Amefahamisha kuwa kama serikali ya CCM ilivyoshiriki harakati za kupigania haki na usawa mahali popote dunia ambako haki ,usawa na uhuru wa watu ulifungwa vitanzi, vikwazo vya kiuchumi dhidi zimbabwe pia havipaswi kuwepo.
'Hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa Kwa niaba ya Mhe Rais Magufuli ilikuwa ya kijasiri na kizalendo . CCM mkoa wa Morogoro tunaungana na Mwenyekti wa CCM Dkt Magufuli kwanza tuitaka dunia ijikinge na virusi vya Corona. Pia wito wetu dunia ikatae fedheha inayoipa mateso zimbwebwe dhidi ya vikwazo vya kiuchumi kwa nchi hiyo na kutatiza "Alisema Shaka
Aidha Katibu huyo alisema vikwazo hivyo vikiendelea kubaki ni kama kuifunga upya Zimbabwe minyororo inayominya uhuru wake, kuinyima fursa muhimu huku vikwazo hivyo vikiwa ni adhabu na ukandamizaji wa haki unaoinyemelea nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
"Kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya kiuchumi ni kuilundikia mzigo wa mateso Zimbabwe bila hatia .Kibinadamu haipaswi tena kuwashuhudia wazimbabwe wakiishi kwa mashaka huku nchi za sadc zikiitazama nchi hiyo na watu wake wakiteketea kiuchumi na maradhi" Alisema
Shaka alisema Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe haikustahili arithishwe vikwazo hivyo badala yake ingekuwa uungwana akapewa nafasi na fursa ili atekeleze sera zake , kutoa ushirikianao kidiplomasia na kufanyakazi za kimahusiano na taasisi za kidunia.
"Ni vikwazo haramu vya kiuchumi vyenye maonevu na fedhuli. Wakati huu dunia ilipaswa kujali utu wa kila mmoja duniani .Ni wakati wa kupambana na virusi vya Corona na kuonyesha mshikamano. Vikwazo kwa zimbabwe havijengi ustawi wala havina maana yoyote " Alisisitiza Shaka
Hata hivyo Katibu huyo alisema ni jambo la kufurahisha kumuona Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Magufuli, akiendeleza msimamo wa kupigania haki na utu duniani huku ukizitaka nchi za sadc kusimama pamoja na kuzidisha ari ya mapambano na kupinga aina yoyote ya ukandamizaji haki
0 comments:
Post a Comment