Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa bunge, Job Ndugai (wa pili kushoto ) wakishuhudia wakati viongozi wa dini walipotia saini Tamko Rasmi la Viongozi wa Juu wa Taasisi za Dini kuhusu ushiriki wao katika mwitikio wa UMKIMWI nchini, wakati Waziri Mkuu alipozindua kampeni ya kitaifa ya viongozi wa dini na bunge katika kupunguza unyanyapaa dhidi ya UKIMWI kwenye ukumbi wa Msekwa bungeni jijini Dodoma, Machi 10, 2020. Viongozi waliotia saini kutoka kushoto ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Zubeir Bin Ali Mbwana, Askofu Peter Konki kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, Akofu Mkuu wa Jimbo la Mbeya na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Gervas Nyisonga, Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini mwa Tanzania wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, Mark Malekana na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya Kikristo Tanzania, Askfu Dkt. Alinikisa Cheyo. Kushoto kwa Waziri Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na UKIMWI, (NACOPHA), Leticia Kapela na kulia kwa Spika ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini na Mkuu wa Kanisa hilo, Dkt. Frederick Shoo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kitabu kutoka kwa Mbunge wa Bunge la Zambaia, Mhe. Princess Kasune ambaye anishi na virusi vya UKIMWI baada ya Waziri Mkuu, kuzungumza wakati alipozindua kampeni ya kitaifa ya viongozi wa dini na bunge katika kupunguza unyanyapaa dhidi ya UKIMWI kwenye ukumbi wa Msekwa, bungeni jijini Dodoma, Machi 10, 2020. Kitabu hicho kiitwacho Warrior Princess kimeandikwa na mbunge huyo kwa lengo la kutoa maarifa kuhusu kuishi kwa mtumaini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment