Waziri
wa Madini Doto Biteko, akijipaka kitakasa mikono baada ya kupimwa joto kwenye
mgodi wa Williamson Diamond Limited alipokuwa kwenye ziara yake Mwadui wilayani
Kishapu mkoa wa Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon
Msanjla akipimwa joto kabla hajaingia kwenye ukumbi wa mkutano katika mgodi wa
Williamson Diamond Limited nyuma yake ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof.
Idris Kikula.
Mkurugenzi wa Mgodi wa Williamson Diamond
Limited, Mhandisi Ayoub Mwenda akielezea jambo mbele ya Waziri wa Madini Doto
Biteko alipokuwa kwenye ziara yake wilayani Kishapu
mkoa wa Shinyanga kushoto mbele ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris
Kikula.
Waziri wa madini Doto Biteko amesikitishwa
na kitendo walichokifanya uongozi wa mgodi wa madini ya Almasi wa Williamson
Diamond Limited (WDL), uliopo Mwadui katika wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
cha kutaka kuuza kinyemela mgodi huo bila
Serikali kupewa taarifa.
Hayo ameyasema leo Julai 5, 2020 na Waziri
wa Madini Doto Biteko alipofanya ziara yake kwenye mgodi huo mara baada ya
kuona matangazo ya kuuzwa kwa mgodi huo kwenye mitandao ya kijamii.
Waziri Biteko, alisema Serikali inaubia wa
asilimia 25 katika mgodi wa WDL, haiwezekani utakekuuzwa bila mmbia wake
kufahamu kitendo hicho ni kukiuka
taratbu na Sheria za nchi.
“Serikali inaubia wa asilimia 25 kwenye
mgodi huu kama mnataka kuuza mgodi lazima mtoe taarifa serikalini na mpate
kibali, kwa mantiki hiyo serikali inapaswa kuwaadhibu kwa kutaka kuuza mgodi
bila kibali huko ni kuhujumu nchi,hivi mlituuliza serikali hatuna uwezo wa
kununua mgodi na kuuendesha?,” alisema Waziri Biteko.
Kutokana na kitendo hicho, Waziri Biteko
ameuagiza uongozi wa mgodi huo kufikia Julai 10 mwaka huu wawe wametoa maelezo
kwa maandishi kueleza sababu za kutaka kuuza mgodi huo bila mmbia wake ambaye
ni Serikali kujua na pia, kutoa taarifa ya kuwapunguza kazi wafanyakazi kisha
kuwalipa nusu mshahara.
Alisema wafanyakazi waliopunguzwa kazi kwa
kutumia kigezo cha ugonjwa wa Corona utaratibu uliotumiwa haufai na wao kama
Wizara ya Madini hawakubaliani nao kutokana na kulipwa mishahara nusu jambo
ambalo linawapa wakati mgumu na kusababisha migogoro isiyo ya lazima.
Aidha, Waziri Biteko, alisema sababu ambazo
wanazitoa mgodi huo za kusitisha shughuli za uzalishaji na kutaka kuuza mgodi
huo ni kushuka kwa bei ya almasi duniani iliyosababishwa na ugonjwa wa corona,
ambapo alieleza kuwa sababu hizo hazina mashiko ila wawe wakweli kama
wamefilisika ijulikane.
Waziri Biteko alisema sababu kubwa ambayo
ingefanya mgodi huo kufungwa ni kushuka kwa uzalishaji na siyo uendeshaji, huku
akihoji kama mgodi hauna fedha za kujiendesha wangesema badala ya kuweka
matangazo kwenye mitandao mgodi unauzwa wakati serikali haina taarifa.
kwenda mitandaoni.
Kwa upande wake meneja mkuu wa mgodi huo
Mhandisi Ayoub Mwenda, alikiri kuwa hawakutoa taarifa Serikalini juu ya kutaka
kuuzwa kwa mgodi huo, huku akieleza kuwa walifunga mgodi huo April 8 mwaka huu
kutokana na kushindwa kujiendesha na ameahidi kufuata maelekezo yote ambayo
yametolewa na Waziri wa Madini.
Mhandisi Mwenda alisema walikuwa
wanazalisha vizuri kabla ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona ambapo kwa mchanga
waliokuwa wameuzalisha walikuwa mbele kwa asilimia tatu na almasi walizokuwa
wamezikusanya walikuwa mbele kwa asilimia 9.1kulingana na bajeti yao waliyokuwa
wameiweka.
Alisema tatizo la Corona limeuathiri sana
mgodi huo na kusimama kufanya shughuli za uzalishaji kutokana na kushuka bei ya
masoko ya nje ambapo kabla ya Corona bei ilikuwa dola 246 kwa karati moja
ambapo Machi mwaka huu waliuza karati moja dola 135 ambayo ilikuwa haiwezi
kutosheleza gharama za uzalishaji.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba
ameipongeza Wizara ya Madini kwa kazi nzuri wanazozifanya ambapo wamesaidia
nchi kuingia katika uchumi wa kati.
0 comments:
Post a Comment