Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 6 Februari 2020 kutoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) (Picha Zote Na Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 6 Februari 2020 kutoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 6 Februari 2020 kutoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) na Mwingine ni Mkurugenzi wa mazao wa wizara ya Kilimo Ndg Nyasebwa Enock Chimagu.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo tarehe 6 Februari 2020 kutoa taarifa kuhusu sekta ya kilimo nchini.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imetangaza kuanza usajili wa wadau
wote katika mnyororo mzima wa uongezaji thamani ya mazao ya kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma
leo tarehe 6 Februari 2020, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema
kuwa Lengo la usajili huo ni kutaka kuwa na takwimu sahihi ya wadau mbalimbali
wanaotoa huduma katika sekta ya kilimo nchini.
Ametaja wadau hao kuwa ni pamoaj na wakulima,
watoa huduma mbalimbali za pembejeo, wasindikaji, wafanyabiashara za mazao,
Taasisi za fedha, watoa huduma wa sekta binafsi katika kilimo kama Asasi za
kiraia na mashirika ya ndani na nje ya nchi
yanayotoa huduma kwenye kilimo, wenye viwanda vya kuongeza thamani,
watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa zana za kilimo n.k.
Amesema kuwa Usajili huo utafanyika kwa njia ya
kidigitali kwenye mtandao wa www.kilimo.go.tz na kupitia simu za kiganjani.
Waziri Hasunga amesema kuwa Usajili huo utaanza
rasmi tarehe 15 Februari, 2020 na kukamilika tarehe 14 Aprili, 2020.
Kupitia usajili huo, takwimu na taarifa muhimu
zitapatikana kwa ajili ya kuendeleza kilimo zikiwemo watoa huduma za pembejeo,
huduma za ugani, taasisi za fedha, wasindikaji na wenye viwanda, watengenezaji,
wauzaji, wasambazaji wa zana za kilimo, na hivyo, kuweza kujua kiwango cha
uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Mhe Hasunga amesema kuwa Wizara ya kilimo
inaendelea na usajili wa wakulima kote nchini ili kuweza kuwatambua na
kurahisisha utoaji wa huduma za ugani, mitaji kwa ajili ya kilimo, upatikanaji
wa pembejeo na kupata taarifa sahihi za uzalishaji.
Amesema kuwa Usajili wa wakulima Awamu ya
Kwanza hadi kufikia Januari, 2020 umefikia jumla ya wakulima 1,279,884 na usajili unaendelea.
Kati yao, wakulima wa mashamba makubwa ni 147 wakewemo 101 wa zao la kahawa, chai
12, Mkonge 22 na miwa 12; na wakulima wadogo ni 1,279,737 wakiwemo 309,000 wa zao la Korosho (98.4%), 305,260 wa Kahawa (95.4), Pareto 10,687 (112%),
Mkonge 6,885 (91%), miwa wakulima 6,745 (96.4), chai wakulima 31,092%, Tumbaku
wakulima 53,757 (107.5%) na Pamba wakulima 556,306 (92.7).
Usajili wa wakulima Awamu ya Pili utaanza kwa
kutumia mfumo wa kidigitari kwa kusajili taaarifa muhimu za wakulima ikiwemo
ukubwa wa mashamba yao, aina ya teknolojia wanazotumia katika uzalishaji, wadau
wanatoa huduma za kifedha, huduma za ugani, pembejeo, n.k
Waziri Hasunga
amesema kuwa Maendeleo ya Kilimo hasa katika kuongeza uzalishaji na tija kwa
wakulima yanategemea kwa kiasi kikubwa matumizi sahihi ya mbegu bora, mbolea na
viuatilifu.
Licha ya umuhimu
huo, bado kuna changamoto ya upatikanaji na matumizi sahihi ya pembejeo hizo ikilinganishwa
na mahitaji.
Aidha, inakadiriwa
kuwa wakulima nchini wanapoteza takribani asilimia 30 ya mazao kabla na baada
ya mavuno kutokana na magonjwa na milipuko ya visumbufu mbalimbali vya mimea.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment