METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, February 29, 2020

MTENDAJI AHUJUMU ZIARA YA MKUU WA MKOA WA IRINGA

mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wananchi wa kata ya Itandula tarafa ya Kasanga wilani Mufindi wakati wa ziara ya Iringa mpya wamu ya Pili

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mtendaji wa kata ya Itandula tafara ya kasanga amehujumu ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi kwa kuwakataza wananchi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa huyo.

Hayo yamebaika wakati wa ziara hiyo ambao Paroko wa kanisa la kijiji cha Nyigo aliposisima na kumwambia mkuu wa mkoa kuwa anahujumiwa katika ziara hiyo na baadhi ya watendaji ambao sio waaminifu na waadilifu.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyigo,Paroko Sylvester Makungu alisema kuwa wananchi wametishwa na kukataza kuuliza maswali na baadhi ya viongozi ndio maana unaona kwenye mstari wananchi sio wengi kutokana na uoga uliopo.

“Hapa wananchi wanakero nyingi na wanahamu ya kuuliza maswali ila viongozi hawa unaowaona mbele hapa wameitisha vikao kabla hujafika na kuwakataza wananchi wananchi wasiulize maswali yanayowahusu wao” alisema

Paroko Sylvester aliwataja wanaohujumu ziara hiyo kuwa ni viongozi wa kata Itandula na tarafa Kasanga kwa kuitisha vikao ambavyo sio rasmi lengo likiwa kuhakikisha wananchi hawapati nafasi ya kuuliza swali ambalo kwa namna moja au nyingine linawahusu wao.

Akijipia hoja hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa,afisa tarafa wa tarafa ya Kasanga Daniel Dugange alikiri kuwepo kwa vikao hivyo pamoja na zuio hilo kwa wananchi na jambo hilo lilifanywa na mtendaji wa kata.

“Nilipofika hapa nilikutana na vikao hivyo lakini mimi nilikataa na kuwaamuru wananchi wawe na uhuru wa kuuliza maswali kwako kwa kuwa walikuwa na hamu ya kukuona na kuuliza maswali ili watatuliwe kero zao” alisema Dugange

Kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Itandula alikiri kufanya kosa hilo na kuomba msamaa kwa mkuu wa mkoa kuwa alifanya kosa hilo.

Naye mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema kuwakataza wananchi kuuliza maswali ni kuhujumu ziara za kiserikali zenye lengo la kutatua kero za wananchi wanyonge kwa kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa na lengo la kutatua kero za wananchi.

Hapi aliongeza kuwa kufanya hujuma kama hivyo ni kuwaongezea hasira wananchi juu ya serikali ya awamu ya tano jambo ambao halina ukweli huo hivyo viongozi wanatakiwa kutatua kero za wananchi na kuwafanya wananchi waipende serikali yao.

Aidha Hapi aliamua kumusamee mtendaji huyo na kutoa onyo kali kuwa asije akarudia tena kuwa nyima haki wananchi walioiweka madarakani serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr John Pombe Magufuli.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com