mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi akiongea na wananchi wa kata ya Itandula tarafa ya Kasanga wilani Mufindi wakati wa ziara ya Iringa mpya wamu ya Pili
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mtendaji
wa kata ya Itandula tafara ya kasanga amehujumu ziara ya mkuu wa mkoa wa Iringa
Ally Hapi kwa kuwakataza wananchi kutoa ushirikiano kwa mkuu wa mkoa huyo.
Hayo yamebaika
wakati wa ziara hiyo ambao Paroko wa kanisa la kijiji cha Nyigo aliposisima na
kumwambia mkuu wa mkoa kuwa anahujumiwa katika ziara hiyo na baadhi ya
watendaji ambao sio waaminifu na waadilifu.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyigo,Paroko Sylvester
Makungu alisema kuwa wananchi wametishwa na kukataza kuuliza maswali na baadhi
ya viongozi ndio maana unaona kwenye mstari wananchi sio wengi kutokana na uoga
uliopo.
“Hapa wananchi
wanakero nyingi na wanahamu ya kuuliza maswali ila viongozi hawa unaowaona
mbele hapa wameitisha vikao kabla hujafika na kuwakataza wananchi wananchi
wasiulize maswali yanayowahusu wao” alisema
Paroko
Sylvester aliwataja wanaohujumu ziara hiyo kuwa ni viongozi wa kata Itandula na
tarafa Kasanga kwa kuitisha vikao ambavyo sio rasmi lengo likiwa kuhakikisha
wananchi hawapati nafasi ya kuuliza swali ambalo kwa namna moja au nyingine
linawahusu wao.
Akijipia
hoja hiyo mbele ya mkuu wa mkoa wa Iringa,afisa tarafa wa tarafa ya Kasanga
Daniel Dugange alikiri kuwepo kwa vikao hivyo pamoja na zuio hilo kwa wananchi
na jambo hilo lilifanywa na mtendaji wa kata.
“Nilipofika
hapa nilikutana na vikao hivyo lakini mimi nilikataa na kuwaamuru wananchi wawe
na uhuru wa kuuliza maswali kwako kwa kuwa walikuwa na hamu ya kukuona na
kuuliza maswali ili watatuliwe kero zao” alisema Dugange
Kwa upande
wake mtendaji wa kijiji cha Itandula alikiri kufanya kosa hilo na kuomba msamaa
kwa mkuu wa mkoa kuwa alifanya kosa hilo.
Naye mkuu
wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alisema kuwakataza wananchi kuuliza maswali ni
kuhujumu ziara za kiserikali zenye lengo la kutatua kero za wananchi wanyonge
kwa kuwa serikali ya awamu ya tano imekuwa na lengo la kutatua kero za
wananchi.
Hapi aliongeza
kuwa kufanya hujuma kama hivyo ni kuwaongezea hasira wananchi juu ya serikali
ya awamu ya tano jambo ambao halina ukweli huo hivyo viongozi wanatakiwa
kutatua kero za wananchi na kuwafanya wananchi waipende serikali yao.
Aidha Hapi
aliamua kumusamee mtendaji huyo na kutoa onyo kali kuwa asije akarudia tena
kuwa nyima haki wananchi walioiweka madarakani serikali ya awamu ya tano chini
ya Rais Dr John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment