Na Mwandishi Wetu Morogoro
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya- Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. John Jingu akitoa maelezo kuhusu Sera ya Wazee ya mwaka 2003 ambayo
inafanyiwa mapitio ili kuiboresha wakati alipofungua kikao cha wadau wanaoshughulikia huduma na haki za
wazee kwenye ukumbi wa Chuo cha VETA jijini Dodoma.
Baadhi
ya wadau mbalimbali wanaoshiriki kikao kazi cha kuhuisha Sera ya Wazee
wakifuatilia mwongozo wa utoaji maoni ili kuboresha sera hiyo katika ukumbi wa VETA jijini Dodoma.
Dkt. Jingu alisema hayo wakati wa kufungua Kikao
cha wadau wa Kitaifa waliokutana jijini Dodoma kwa lengo la kuhuisha Sera ya
Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 ambayo inapitiwa, kujadiliwa na kupokea maoni kuhusu
uhalali wa matamko na maelekezo ya kisera kwa ajiliya kuboreshwa ili kuwapa
fursa ya kuendelea kutoa mchango katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha Dkt. Jingu amebainisha kuwa Mtaalam
mwelekezi Dkt. Richard Sambaiga ameandaa rasimu ya awali ya Sera hiyo itatumika
kuchochea fikra za wadau ili kupata maoni chanya yatakayojumuishwa katika Sera
iliyoboreshwa maana itazingatia mazingira halisi ya afya, ulinzi, usalama,
hifadhi ya kijamii, matunzo na ushirikishwaji katika masuala ya kijamii.
Katika kutkeleza Sera ya Wazee ya Mwaka 2003,
Dkt. Jingu ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za
kuhudumia wazee ikiwa ni pamoja na kusimamia makao ya wazee 17 ya
yanayomilikiwa na Serikali ambayo hivi sasa yamepunguzwa manne na kubaki 13 kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wazee
wasiojiweza wanaoishi katika makao hayo baada ya familia zao kushindwa kuwapa
huduma za msingi.
’’Katika mazingira ya kawaida Serikali
inachukua jukumu la kuwalea wazee baada ya kuthibitika kuwa familia husika
haina uwezo au haikujitokeza kutoa huduma’’. Aliongeza Dkt. Jingu.
Aidha
Dkt. Jingu amesisitiza kuwa wajibu wa kulea wazee wasio jiweza sio haukomei tu
kwa familia bali ni jukumu linalohussha pia jamii kwa ujumla hivyo amewataka
wadau wote kutambua kuwa kila mtu anamchango katika malezi na matunzo ya wazee hapa nchini.
Kadhalika, Mpango wa utambuzi
wa wazee katika Halmashauri hadi kufikia Desemba, 2019 umewezesha
kuwatambua jumla ya Wazee 1,837,162 (Me
834,595 na Ke 1,002,567). Kati yao wazee wasio na uwezo 684,383 (ME:348,171,
KE:336,212) wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bila malipo.
Naye Kamishina wa Ustawi
wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi ameeleza kuwa ni muhimu kuboresha Sara ya wazee ili
kuakisi mahitaji na changamoto zinazowakabili wazee kwa kuatika mazingira ya
sasa maana sera iliyopo ni ya miaka16 iliyopita.
Dkt. Ngondi ameongeza kuwa azma ya kikao cha
wadau wanaosimamia na kushughulikia masuala ya huduma na haki za wazee
watajadili kwa pamoja na na kupendekeza namna sera pendekezi itaweza kuzingatia
maeneo ya msingi.
Aidha Mtaalam mwelekezi anayeandaa Sera ya
Wazee Dkt. Richard Sambaiga aliwambia washiriki kuwa suala la uzee na kuzeeka
sio suala la kupuuzwa tena bali ni jambo ambalo linahitaji kuzingatiwa katika
mipango ya maendeleo ya kisekta maana idadi ya wazee hapanchini ambayo ni
takriban asilimia 5.6 itaongezeka mara tatu ifikapo mwaka 2050 maana uwekezaji
unaofanyika unaongeza idadai ya wazee na kupunguza umasikini uliokithiri.
Itakumbukwa kuwa wazee wanatambulika kuwa ni walinzi wa
mila na desturi, washauri/wapatanishi, na walezi wa watoto wadogo hivyo Sera
inayoboreshwa itaweka matamko ambayo yatahakikisha wazee wanathaminiwa katika
jamii kwa kuwa, uwepo wa Taifa la
Tanzania ni kielelezo tosha cha mchango mkubwa wa utumishi wa wazee katika
nyanja mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment