Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Constantine Kanyasu akionesha eneo la Pori Tengefu akiwa kwenye kigingi
ambacho ni mpaka kati ya eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la
mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la
Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji
hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya
Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa
wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani
Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
wakiwa kwenye eneo la kigingi huku Mbunge huyo akiomuonesha Naibu Waziri
Kanyasu eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya
wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo
limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio
sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo
lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka
katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Baadhi ya wananchi wakiwa na Naibu Waziri
wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakiangalia eneo la
Kihurumila sehemu ambayo kuna mto na ambalo lilikuwa na mgogoro kuwa sio
mali ya pande zote mbili bali mali ya serikali kuu inayomilikiwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mbunge wa Liwale, Mhe.Zuberi Kuchauka
akizungumza na wananchi wake kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa ardhi
uliodumu kwa miaka 12 baada ya Naibu Waziri Kanyasu kuzungumza na
wananchi hao
Baadhi ya wananchi wakiwa wanatoka eneo
lenye mgogoro ambapo walitaka eneo hilo la mto waweze kilitumia kwa
ajili ya kulishia mifugo pamoja na kulima katika mto huo ambapo kutokana
na hali hiyo mto huo usingeweza kudumu kwa muda mrefu
Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock
Msocha ( kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine Kanyasu wakati walipotembelea eneo amvalo lilikuwa na
mgogoro kati ya Kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous
Aniel Heliem mmoia wa wananchi akimuuliza
swali Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Cinstantine Kanyasu mata
baada ya kuutangaza kuwa eneo la Kihurumila si sehemu ya Pori la Akiba
la Selous na wala sio eneo la Kijiji cha Kikulyungu.
…………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Constantine Kanyasu ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 12 baina ya
Pori la Akiba la Selous na Wananchi wa kijiji cha Kikulyungu kilichopo
katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Mgogoro huo wa ardhi ulianza mwaka 2007
ambapo wananchi walianza kudai kuwa eneo la Kihulumira ambalo
linapakana na Pori la Akiba la Selous kuwa ni moja ya maeneo yao ya
Asili.
Kufuatia hali ilipelekea uhasama mara kwa
mara kati ya wananchi na askari wanyamapori hasa pale wananchi
walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa wameingia ndani ya Hifadhi bila
kibali.
Akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha
Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo lililokuwa na mgogoro, Kanyasu
alisema eneo hilo lilisajiriwa mwaka 1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka
2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya kijiji.
Amesema baada ya kuundwa timu hiyo
iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazo ilibainika kuwa eneo hilo si la wananchi
na wala sio sehemu ya Pori la Akiba la Selous bali ni Pori Tengefu
ambalo ni mali ya serikali Kuu na linasimamiwa na Wizara ya Maliasili
na Utalii.
Katika hatua nyingine, Kanyasu amewataka
wananchi kuacha vitendo vya kukata miti ovyo na kuchoma misitu kutoka
na uharibifu mkubwa wa misitu aliuona karibu na eneo lililokuwa na
mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu
amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo kuweka sheria kali ili kudhibiti
hali ya uharibifu wa misitu unaoendelea katika maeneo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wanachi wa
wilaya ya Liwale Mbunge Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru serikali
kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa
haujapatiwa ufumbuzi
Amesema mgogoro huo uliwafanya wananchi
wa maeneo hayo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo badala yake wajanja
wachache walikuwa wakitumia nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.
” Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi” Alisisitiza Kuchauka.
Kutokana na kumalizika kwa mgogoro huo
wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kulitumia eneo hilo
kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ili kuinua kipato katika
kijiji hicho
0 comments:
Post a Comment