"Kusimamia mageuzi na kupata maendeleo ya kweli kunahitaji uthubutu, umakini na moyo mgumu ili kujikomboa kiuchumi, kijamii na kisiasa katika Taifa" Shaka
"Yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano ni mambo muhimu kwani yanalenga kuwaletea neema ya kudumu watanzania na kuwaondoa kwenye adha na aibu ya kuwa ombaomba" Shaka
"Kulingana na misingi ya historia, mageuzi yaliofuzu popote duniani yalitokana na juhudi za wananchi kuwa na kiongozi makini na mwenye maamuzi magumu kwa niaba Taifa lake" Shaka
"Mapambano ya kisiasa yalioleta Uhuru 1961 na Mapinduzi 1964 hayakudondoka kama mvua, bali wapo waliojitolea na hata kuyaweka rehani maisha yao ili jamii ijikomboe na kuwa huru" Shaka
"Harakati za vyama TANU na ASP hata wazee wetu waliamua kwa sauti moja, wakaamini katika ukombozi hadi uhuru ukapatikana hivyo Tanzania tunatekeleza dhana ya uhuru na ukombozi wetu kwa vitendo chini ya Jemedari John Pombe Joseph Magufuli" Shaka
"Kusimamia mageuzi si kazi nyepesi kama kucheza lelemama au singeli. Kunahitaji mtu awe na roho ya paka ili kufikia mafanikio, wanamorogoro tunathamini sana kazi mnayoifanya viongozi wetu mkiongozwa na Jemedari Dk John Pombe Magufuli" Shaka
"Yapo mambo yanafanyika hivi sasa hayajawahi kutokea. Ni mambo ya manufaa kwetu wote .Kwa wakati uliopo na ujao CCM Morogoro tufikishie salam zetu kwa Mhe Rais Magufuli aendelee tu kuchapa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa sisi zetu ni sala na dua kwake" Shaka
"Serikali imekomesha urasimu na umwinyi . Rushwa, maonevu na manyanyaso sambamba na wizi na ufisadi wa mali za umma, haya yanayofanyika katika kuchukua hatua kali leo kila mmoja ni shahidi endeleeni kuchapa kazi nasisi wasaidizi wenu na wananchi tunawaunga mkono" Shaka
"Mahusiano ya Chama na Serikali Morogoro ni mazuri sana, tumejipanga vyema katika vita ya kisiasa kwa mashambulizi ya ardhini na angani, malengo yetu kuelekea uchaguzi wa 2019 na 2020 kushinda mitaa, vijiji na Vitongoji, 99.9% kushinda viti vya ubunge, udiwani na kuongeza kura za Rais Magufuli 99.9% tutawanyoa vipara wapizani saa 12 asubuhi" Shaka
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Morogoro leo 6 Agosti 2019 kuanza ziara ya siku tatu mkoani hapa alipokelewa na viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi ngazi ya mkoa na wilaya.
0 comments:
Post a Comment