METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 22, 2020

STAMICO KUANZISHA MRADI WA KUSAFISHA DHAHABU MWANZA

Waziri wa Madini Doto Biteko akiieleza jambo Kamati ya Kudumu ya Nishati na
Madini wakati wizara ilipowasilisha kwa kamati hiyo Taarifa kuhusu
Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa Fedha za Maendeleo ya STAMICO kwa
Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan
Kitandula akieleza jambo baada ya Wizara kuwasilisha kwa kamati hiyo Taarifa
kuhusu Utekelezaji na Hali ya Upatikanaji wa Fedha za Maendeleo ya STAMICO
hilo kwa Kipindi cha Nusu Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.

Imeelezwa kuwa, Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) lipo katika hatua za awali
za uanzishwaji wa Mradi wa Kusafisha Dhahabu (Gold Refinery) na tayari
kampuni ya ubia ijulikanayo kama Mwanza Precious Metals Refinery Company
Limited imeanzishwa.

Hayo yamebainishwa leo Januari 21, 2020 na Kaimu Mtendaji Mkuu wa
(STAMICO) Dkt. Venance Mwase wakati akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Nishati na Madini Taarifa kuhusu Utekelezaji na Hali ya
Upatikanaji wa Fedha za Maendeleo ya shirika hilo kwa Kipindi cha Nusu
Mwaka, kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 kwa niaba ya Waziri wa Madini.

Dkt. Venance ameileza kamati hiyo kuwa, mradi huo utaendeshwa kwa ubia
ambapo STAMICO itakuwa na hisa asilimia 25 na mwekezaji asilimia 75, huku
ikilelezwa kwamba, mradi huo utakaojengwa jijini Mwanza utahusisha kujenga
mtambo wenye uwezo wa kusafisha wastani wa kilo 200 hadi 500 kwa siku.
Ameongeza kuwa, makadirio ya fedha zinazohitajika ni Dola la Marekani
Milioni 58.204 ambazo zimepangwa kwa ajili ya ununuzi wa mtambo wa
kusafishia dhahabu, gharama za awali za mradi, kununua dhahabu kutoka
katika masoko pamoja na gharama zaza uendeshaji na kuongeza

‘’ MheshimiwaMwenyekiti tumepanga uwe mtambo wa viwango vya kimataifa,’’.
Aidha, Dkt. Mwase amesema kwamba katika kipindi cha Julai hadi Desemba,
2019, tayari mradi umetekeleza majukumu kadhaa ikiwemo kupata leseni ya
kujenga na kuendesha mtambo huo, kusainiwa mkataba wa ubia pamoja na
kuanza taratibu za uanzishwaji wa kampuni ya ubia na kupata eneo la ujenzi
wa mtambo chini EPZA.

Ameongeza majukumu mengine yaliyotekelezwa ni pamoja na kufanyika kwa
Athari kwa Mazingira (EIA) kwenye eneo la mradi upembuzi yakinifu pamoja na
kukusanya taarifa za upatikanaji wa dhahabu katika maeneo mbalimbali
yanayokusudiwa.

Akizungumzia shughuli nyingine zinazoendeshwa na Shirika hilo amesema
linaendelea kutoa huduma za Kibiashara za uchorongaji miamba wa biashara
katika sekta ya mafuta na gesi ambapo katika Mwaka wa Fedha 2019/20
ambapo limefanikiwa kupata kandarasi 4 za uchorongaji kupitia zabuni
mbalimbali zenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 .

Kuhusu Mgodi wa Stamigold ambao ni Kampuni Tanzu ya Shirika hilo ameieleza
kamati hiyo kuwa, kuanzia Julai hadi |Desemba, 2019, mgodi huo umezalisha

na kuuza wakia 7,133.00 za madini ya dhahabu na wakia 879.19 za madini ya
fedha, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 24,172,700,255.34.

‘’ Mhehimiwa Mwenyekiti, katika kipindi hicho, mgodi umelipa jumla ya shilingi
1,712,455, 550.91 kwa ajili ya malipo ya mrabaha, ada ya ukaguzi na kibali cha
kusafirisha madini nje ya nchi,’’ ameeleza Dkt. Venance.

Kuhusu mradi wa makaa ya mawe katika Mradi wa Kabulo na Kiwira, amesema
jumla ya tani 4,359.10 ziliuzwa na kulipatia Shirika kiasi cha shilingi
17,558,184.76 na kuongeza kuwa,

 ‘’ shirika lilifanikiwa kulipa mrabaha, ada ya
ukaguzi na tozo ya Halmashauri ya jumla ya shilingi 23,645,000.62
Aidha ameongeza kuwa Mgodi umeendelea kutoa ajira kwa Watanzania zaidi
ya 400.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko wakati akitoa ufafanuzi wa
hoja zilizoibuliwa na kamati, amewatoa Hofu Wajumbe wa kamati hiyo kuhusu
Maendeleo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambapo ameeleza pamoja
na changamoto zinazolikabili, linakua na linafanya vizuri.

Waziri Biteko ameiomba Kamati hiyo kuendelea kuilea na kuishauri STAMICO
kwa kuwa mwelekeo wake ni mzuri na kwamba hivi sasa lina uwezo wa
kuzalisha hadi shilingi Bilioni 20 tofauti na ilivyokuwa awali na kuongeza kuwa,
Watendaji na Bodi ya Shirika hilo mara zote wanafanyia kazi ushauri
unaotolewa na Kamati pamoja na Wizara.

‘’Mheshimiwa Mwenyekiti, itakuwa bahati mbaya sana kulifuta shirika hili.
Linakua, wanaendelea vizuri na Wana Bodi nzuri, watendaji wanasikiliza
ushauri na kuufanyia kazi na mapungufu yanafanyiwa kazi, naomba muendelee
kuilea na kuishauri STAMICO,’’amesisitiza Waziri Biteko.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com