METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 22, 2020

NAIBU WAZIRI SHONZA ATOA MAELEKEZO KWA WASANII WA FILAMU MANYARA

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana
Shonza (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Babati Bibi.Elizabeth Kitundu
(kulia) alipowasili katika ofisi ya mkuu huyo leo kwa lengo la kukutana na wadau wa
tasnia ya filamu wa mkoa wa Manyara kukisikiliza kero zao kuwaeleza mikakati ya
serikali katika kuboresha tasnia hiyo.

:Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana
Shonza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Manyara na kuwasisitiza
kujisajili kama ilivyoutaratibu wa kisheria alipofanya kikao na wadau hao leo, kwa
lengo la fahamu changamoto zao na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuboresha
tasnia hiyo.

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
amewataka wasanii wanajisajili kama ilivyoutaratibu ilikuendesha shughuli za usanii
katika mfumo rasmi na msanii anaweza kujisajili katika Halmashauri yake kupitia Afisa
Utamaduni bila kwenda Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Shonza ametoa wito huo leo Mkoani Manyara katika Wilaya ya Babati
Mjini alipofanya kikao na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la
kufahamu kero zao na kuweza kujibu hoja mbalimbali pamoja na kuwaeleza mikakati
ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo.

“Serikali inajipanga kuanzisha Kanzi Data ya wasanii wa tasnia mbalimbali nchini hivyo
basi ni vyema mkajisajili , kumekuwa na changamoto ya kujua wanatasnia wa filamu
wangapi wanafanya kazi kama Uandaaji wa Filamu,Uongozaji wa Filamu na Uandaaji
wa Miswada ya Filamu kwani zipo fursa mbalimbali zinajitokeza lakini namna ya
kuwafikishia wadau hao inakuwa changamoto,”alisema Mhe.Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Mhe.Shonza pia aliwasihi wasanii vijana
wa mkoa huo kujiunga katika vikundi na kwenda katika Halmashauri zao kuchukua
mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kujikwamua kiuchumi hiyo nifursa
kwao na wasiiache ipote sababu serikali inajali vijana hivyo waache kulalamika na
kuomba kusaidiwa kwani mikopo hiyo ipo na haina riba.

Pamoja na hayo na Kaimu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo
aliwaeleza wasanii hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo kwa
kuwaeleza kuwa tayari wameanza utaratibu wa kuimarisha mfumo wa usambazaji wa
kazi za filamu kwa kuhamia mfumo wa digitali ambapo filamu zinaanza kuangaliwa
katika kumbi za sinema na zoezi la kuziweka katika CD na DVD ni hatua ya mwisho
ambapo msanii anakuwa ameshapata faida yake.

“Bodi imeendelea kutangaza fursa kwa wadau mbalimbali watakao ungana na wasanii
watanzania kufanya nao filamu zenye ubora na tayari nchi mbalimbali zimejitokeza
ikiwemo Namibia pia wasambazaji wa mfumo wa kidigitali kama Swahiliflix na Netflix
lengo ni kuhakikisha tasnia inakuwa na tunakomesha uharamia wa kazi za filamu na
wasanii wananufaika na kazi zao,”alisema Dkt.Kiango.

Hata hivyo nae Afisa Utamaduni Mkoa wa Manyara Bi.Frida Nkarange aliwasisitiza
wadau hao wa tasnia ya filamu kuhakikisha wanakuwa karibu na maafisa utamaduni
wa maeneo yao ili waweze kuwapa ushauri na kuhakikisha wanaudhuria vikao
vinavyowahusu kwani vinamanufaa kwa kazi zao.

Halikadhalika Katibu wa Chama cha Wasanii Mkoa wa Manyara Bw.Dulla ambaye ni
msanii wa muziki aliwasisitiza wasanii wenzake kujituma na kuandaa kazi nzuri
zilizozingatia ubora kwani hizo ndiyo zitakazo watangaza na kuwapa heshima badala
ya kulalamika kuwa wanadharauliwa kwani msanii mwenye kazi nzuri lazma
ataheshimika.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com