METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 25, 2017

DC KASESELA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA DARAJA LA TAGAMENDA

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela alipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Tagamenda



Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Tagamenda linalofadhiridhiriwa na serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la DFID. wakati wa ziara hiyo aliyoongazana na Mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Dr William Mafwele. 

Akipokea taarifa ya kazi, alialifiwa kuwa Mhandisi msimamizi wa Mradi amekuwa kikwazo cha utendaji na utekelezaji wa majikumu ikiwemo hata kunyanyasa wafanyakazi. 

Ndio maana mradi umekuwa unasua sua. Mkuu wa wilaya aliamuru Mhandisi Raymond Swai aondolewe haraka na asikanyage kabisa eneo la mradi akionekana mita 100 achukuliwe hatua. " OCD mtafute haraka Raymond Swai mpe amri amri hii kama anabisha atatakiwa aondoek Iringa" Alisema Mkuu wa wilaya. muda huo saa 5 asubuhi bado Mhandisi huyo alikuwa hajafika kazini kufanya kazi zisianze kwa wakati. Mkurugenzi wa Manispaa Dr Mafwele aloinyesha wasiwasi wa mradi kumalizika kwa wakati kwani mkandarsai amekuwa anaishiwa vifaa mara kwa mara .

Mkuu wa wilaya alimuagiza Mkandarasi kuleta vifaa haraka wiki ijayo atapita kukagua tena. Mradi huo wenye thamni wa 5.3bilioni unatarajiwa kukamilika mwisho wa mwezi wa 3 kama makandarasi atafuata ratiba.​
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com