METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, January 25, 2017

DC MUWANGO ATEMBELEA NYUMBA ZILIZOEZULIWA NA UPEPO WILAYANI NACHINGWEA


 Miongoni mwa nyumba zilizoezuliwa na upepo Wilayani Nachngwea Mkoani LIndi

Na Mathias Canal, Lindi

Mvua iliyoambatana na upepo imeleta athari kwa baadhi ya kaya zilipo katika kijiji cha Chiwindi Mkoani Lindi huku mtu mmoja akiumia na kulazwa hospitalini.
 
Akizungumza mbele Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango mtu huyo ambae kwa sasa ameruhusiwa kutoka hospitali kutokana na afya yake kuendeleea kimarika alisema kuwa kisa hicho kimeleta huzuni kwa wananchi waliopatwa a mkasa wa kuezuliwa kwa nyumba zao na kubomoka kutokana na upepo mkali ulombatana na mvua kali.
 
Wahanga wa tukio hilo ni Twahili Swalehe, Halidi Saidi, Jimmy Chilumba na Mwajuma Hassani ambao wote wamepata hifadhi kwa ndugu na majirani huku wakijipanga kwa ujenzi na kurejea kwenye makazi yao.

Mh Rukia Muwango amefika eneo la tukio kwa lengo la kuwapa pole wahanga, mbali na kuwapa pole Mh Rukia amesisitiza kujenga nyumba kwa kuzingatia ujenzi bora huku akiwataka wananchi kuwatumia wataalamu wa ujenzi waliopo wilayani Nachingwea kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza kujenga nyumba zao.

Mhe Muwango amesema kuwa njia pekee ya kuwausuru wananchi katika kadhia kama hizo ni kuwashauri kuwatumia wataalamu mbalimbali katika Wilaya hiyo ili kupata msaada wa kitaalamu juu ya ujenzi bora na wa kisasa wa nyumba zao kwa gharama nafuu.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com