Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb) kulia,
akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb), katikati, na Mkurugenzi
wa Uchaguz, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,
Wilson Mahera, (kushoto) wakati kamati hiyo ilipokagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020,
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb) na Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe.
Aeshi Khalfan Hilaly (Mb), pamoja na
Mkurugenzi wa Uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Wilson Mahera, wakimsikiliza
meneja wa Mradi huo, Godwin Maro, wakati
kamati hiyo ilipokagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume hiyo zilizopo eneo
la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020,
Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb)
katikati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb),kulia pamoja na
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu
na Bunge), Tixon Nzunda wakifuatilia hoja za wabunge wakati wa kikao
na viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kabla ya kamati hiyo kukagua hatua
za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi
za Tume hiyo zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Hesabu za Serikali, wakifuatilia hoja za kikao na viongozi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu kabla ya kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020,
Baadhi ya viongozi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakifuatilia
hoja za kikao na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kabla
ya kamati hiyo kukagua hatua za Mradi wa ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya
Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020,
Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa
mwezi Oktoba mwaka jana, kwa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), ambapo iliitaka Tume hiyo kuhakikisha inasimamia
ukamilishwaji wa Mradi wa ujenzi kwa
wakati wa ofisi za Tume hiyo jijini, Dodoma kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2020.
Akiongea mara baada ya
kukagua hatua ya Mradi wa ujenzi wa jengo
la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma
leo tarehe 15 Februari, 2020, Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe. Aeshi Khalfan Hilaly (Mb), amebainisha kuwa Kamati imeridhishwa
na hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa ofisi za Tume hiyo kwa Jengo Kuu la
Ofisi, Jengo la kutangazia matokeo na ghala la kuhifadhi vifaa.
“Tunaipongeza serikali kwa hatua ilizozichukua kupitia Ofisi
ya Waziri Mkuu katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa Ofisi hizi unakamilika kwa
wakati, kimsingi ni nia njema kamati kutembelea miradi ya serikali lakini
tunapoona inafanya vizuri hatunabudi kuipongeza na ni imani yetu kuwa kwa
malengo iliyoyaweka mwezi Aprili mwaka huu hatua kubwa ya utekelezaji itakuwa
imefikiwa ” Amesisitiza, Mhe. Aeshi
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,
Vijana na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde (Mb) amefafanua kuwa tayari wanatekeleza
maelekezo ya Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa ambaye ameitaka tume hiyo kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa Ofisi za
Tume hizo kwa wakati ili shughuli za uchaguzi za mwaka huu zinafanyika kwenye
majengo hayo.
“Kutokana na mkandarasi mpya wa mradi huu ambaye ni SUMA JKT,
Tumewahakikishia wanakamati wa PAC, kuwa ifikapo mwezi Aprili mwaka huu mradi
wa ujenzi wa ofisi za Tume utakuwa umefikia hatua kubwa kwa kiwango cha
kuruhusu shughuli za Tume kuanza kuendeshwa katika majengo haya, ambapo litakuwa
ni jambo kubwa kwa kuwa katika historia tume hiyo haijawahi kuwa na ofisi yake yenyewe”Amesisitiza
Mhe. Mavunde.
Naye, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge)
Tixon Nzunda, amefafanua kuwa hatua ya ujenzi wa mradi huo imeendelea vizuri
baada ya kutekeleza maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu ya kuvunja Mkataba wa
mkandarasi wa awali wa mradi huo TBA na kusaini mkataba mpya na Kampuni ya
Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelzaji wa Mradi wa Ujenzi
wa Ofisi hiyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wilson Mahera
amebainisha kuwa Tume hiyo kwa kushirikiana na Chuo kikuu- Ardhi na Kampuni ya
Ujenzi ya Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT CCL wanaouhakika mnamo mwezi Aprili
mwaka huu Tume hiyo itaanza kuendesha shughuli zake kwenye majengo hayo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni idara huru iliyoanzishwa mwaka
1993 kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1997, ambapo kwa kipindi chote hicho tangu kuanzishwa kwake Tume hiyo
haijawahi kumiliki Jengo lake lenyewe, hivyo mnano mwaka 2016, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alikubali ombi la Tume hiyokujenga jingo
lake. Dodoma leo tarehe 15 Februari, 2020
0 comments:
Post a Comment