METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 10, 2019

WAFUNGWA 79 WA GEREZA KUU BUTIMBA WALIONUFAIKA NA MSAMAHA WA RAIS WAACHILIWA LEO JIJINI MWANZA


Mfungwa mnufaika wa Msamaha wa Rais, William Dingu akizungumza na
Wanahabari(hawapo pichani) baada ya kuachiliwa huru leo. Mfungwa huyo amemshukru Rais kwa msamha huo, aidha, amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kumwezesha ujuzi wa wa fani ya ujenzi ambao ameupatia gerezani kupitia programu ya Urekebishaji inayosimamiwa na Jeshi hilo. 

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela(vazi la kitenge) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa mwanza alipowasili gereza Butimba kushuhudia zoezi la uachiliaji wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais.
Baadhi ya wafungwa wakiume wa Gereza Kuu Butimba walionufaika na Msamaha wa Rais wakitoka katika lango la Gereza Kuu Butimba tayari kwenda kuungana na familia zao. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo wa kihistoria.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, CGP – Phaustine Kasike akitoa taarifa fupi ya zoezi zima la uachiliaji wa wafungwa walionufaika na msamaha wa Rais katika mikoa mbalimbali nchini mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari jijini Mwanza leo Desemba 10, 2019.
Wafungwa wa kike Gereza Kuu Butimba – Sehemu ya Wanawake wakitoka gerezani baada ya Msamaha wa Rais alioutoa jana katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru. Wafungwa hao wamemshukru Rais Magufuli kwa msamaha huo na wameahidi kutokurejea katika uhalifu.
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Mwanza pamoja na Kamishna Jenerali wa
Magereza nchini, Phaustine Kasike wakishuhudia wafungwa walionufaika na Msamaha wa Rais katika Gereza Kuu Butimba wakipewa mali zao na nauli ya kwenda kuungana na familia zao leo Desemba 10, 2019 kabla ya zoezi la uachiliaji wa wafungwa husika wa msamaha huo.


(Picha zote na Jeshi la Magereza).
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com