Mwenyekiti wa shirika lisilo kuwa la kiserikali linalo jihusisha na masuala ya usaidizi wa kisheria katika manispaa ya Iringa (IPACE) Isaac Kikoti akiongea wakati wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na wanahabari kuhusiana na ukatili wa kijinsia
Baadhi ya washiriki wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi,wadau mbalimbali na baadhi ya wanahabariFREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi
mkoani Iringa wametakiwa kutunza na kuheshimu haki zote za mtoto ili kuepukana
na ukatilii unaendelea kwa watoto kwa kuwalea katika malezi mazuri yenye faida
katika maisha ya baadae.
Hayo yamezungumzwa na afisa wa dawati
la jinsia na watoto Elizabert Swai wakati
wa semina iliyoshirikishwa wenyeviti wa mtaa, mabalozi nyumba kumi na
wanahabari kwa uratibu wa shirika lisilo kuwa
la kiserikali linalo jihusisha na masuala ya
usaidizi wa kisheria katika manispaa ya
Iringa (IPACE).
Swai alisema kuwa wenye viti, wapya
waliopishwa hivi karibuni wametakiwa kuzifikisha tuhuma zozote za ukatili wa
kijinsia katika dawati la jinsia la jeshi la polisi kwa ajili ya upelelezi
zaidi.
Alisema kwamba matukio ya ukatili wa
jinsia yamekuwa yakiongezeka na watu wa Kwanza kukutana nayo ni wenyeviti wa
mtaa hivyo ni muhimu kufikisha hatua za mbele,watoto wengi wamekuwa wakibakwa
au kunyanyaswa kijinsia.
Aidha Swai ametoa wito kwa watu wanaokumbana na matukio ya ukatili wa
kijinsia ikiwemo ubakaji kujitokeza katika kituo cha polisi ndani ya masaa 72
ili kuweza kufanya upelelezi na kutibiwa kama umeambukizwa magonjwa ya
zinaha au ukimwi.
Awali akisoma Risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa shirika
lisilo kuwa la
kiserikali linalo jihusisha na
masuala ya usaidizi
wa kisheria katika manispaa ya
Iringa (IPACE) Isaac Kikoti alisema kuwa katika
siku 16 wamefanikiwa kutoa msaada wa
kisheria kwa wahanga mbalimbali katika
jamii ya watu waishio katika manispaa ya
Iringa ,na walio nje ya manispaa
na wametatua migogoro ya ardhi,ndoa ,mirathi ,matunzo ya watoto na ukatili
wa kijinsia
“Ndoa na ardhi kesi
hizi zimekuwa nyingi katika jamii zimechukua nafasi kubwa katika jamii ya wananchi wa manispaa ya
Iringa na tumefanikiwa kuwasaidia kwa kuwaandikisha wateja wetu katika vitu vya
ushauri kama Mahakamani,Polisi,Ustawi wa jamii na Dawati la jinsia manispaa ya
Iringa” alisema Kikoti.
Alisema kuwa wamefanya utafiti kwa
wanao tendewa vitendo vya ukatili
kwa kuangalia maendeleo yao baada ya mashauri yao kutatuliwa na kugundua wana
endelea vizuri na wamegundua kuwa elimu iliyotolewa kwa wananchi wanatoa ushirikiano
kwa kutoa taarifa.
“vitendo vya ukatili vime pungua katika jamii kwa
asilimia kubwa baada ya watu kupata ushauri kutoka kwa PARALEGAL na jamii imenufaika baada ya elimu wameweza
kujua haki zao za msingi na kuondokana na mila na desturi potofu lakini
wanakuwa wazi kupeleka mashauri katika vyombo vya sheria”alisema Kikoti
Lakini pia Kikoti alizitaja changamoto ambazo
wamekuwa wanakabiliana nazo ni kutokuwa na usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda
sehemu nyingine ili kuifikia jamii kwa ufasaha ,Jamii kutotoa ushirikiano pale
ambapo vitendo vya ukatili na unyanyasaji vinatokea,Mabadiliko ya sheria mpya
ya msaada wa kisheria,pindi ambapo kila msaidizi wa kisheria anapaswa kulipa
ada Tsh 30,000 kwa mwaka na Taasisi kuto kuwa na mradi wa kujiwezesha.
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye semina hiyo mwenyekiti wa kuwasimamia
watetezi wa kisheria Tanzania Bara Eliah Kasanga alisema kuwa serikali ya awamu
ya tano imeanzisha baraza watetezi wa kisheria kwa lengo la kuwasaidia wananchi
wasio na uwezo wa kiuchumi ili nao waweze kupata haki zao.
“Ukifika mahakamani mtafute anayesimamia utetezi wa kisheria utapata
msaada wa kisheria,maana ya mheshimiwa Rais ni kwamba mtu asifungwe kwa sababu
hana uwezo ila ufungwe kwa sababu unakosa nah ii sheria ipowazi inapswa
kusambazwa kwa wenyeviti wote mkoani hapa ili kwasaidia wananchi kupata haki
zao” alisema Kasanga
Na afisa utamaduni wa manispaa ya Iringa Merysina Ngowi alisema kuwa watoto wanaofanyiwa ukatilii wamekuwa
wanaathirika kisaikolojia kutokana na matendo yanakuwa yamewakumba.
Alisema
kuwa watoto wakifanyiwa ukatili wanapata madhara makubwa katika maisha yao
hivyo wananchi wanatakiwa kuheshimu haki za watoto.
0 comments:
Post a Comment