NA
MWANDISHI WETU
MWENYEKITI
wa TANESCO Sports Club , Omary
Shabani amesema kuwa mwaka huu TANESCO imejiandaa kuchukua makombe yote katika
mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma , Taasisi na Makampuni
Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea jijini Mwanza.
Mashindano
ya SHIMMUTA kwa mwaka huu 2019 yanafanyika katika viwanja tofauti huku jijini
humo yakihusisha jumla ya timu 46 ikiwa ni ongezeko la klabu 20 kwani ya mwaka
jana yaliyo fanyika Jijini Dodoma yalikuwa na timu 26.
Akizungumzia
maandalizi ya TANESCO, Shabani alisema maandalizi ya timu zote yamekamilika na
mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja hivyo ndoto ni kuchukua mataji ya
michezo yote inaanza kutimia taratibu.
"Mwaka
Jana kule Jijini Dodoma tulikuwa mabingwa wa jumla, pia msimu huu tunataka
kufanya hivyo na kuongeza vikombe zaidi katika michezo yote ambayo tunashiriki,
maandalizi yalifanyika mazuri , hatuna shaka tutafanya hivyo" alisema
Shaban.
Kwa
upande wake Meneja wa TANESCO katika mchezo wa Netball, Nazareth Mwanjala
alisema mashindano hayo ni muhimu kushiriki kwani husaidia kuleta maendeleo pia
hupelekea kufahamiana miungoni mwa Washiriki hivyo hubadilisha mawazo na uzoefu
wa kazi.
0 comments:
Post a Comment