METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 10, 2019

SERIKALI YAZITAKA TAASISI ZA DINI ZA KIELIMU KUITUMIA TUME YA CSSC



Kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI] Dkt.George Jidamva,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] kwa niaba ya Naibu katibu mkuu TAMISEMI Gerald  Mweli aliyemuwakilisha uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa huduma za Elimu -CSSC Mwl.Petro Pamba ,akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC] uliofanyika leo jijini Dodoma.
  
Sehemu ya washiriki wakifatilia Hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC]
Katibu wa Elimu Jimbo la katoriki la Moshi mkoani Kilimanjaro ,Padri.William  Ruwahi’ch,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi mara baada ya kufungua Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa yaliyo chini ya Kanisa Katoliki na Jumuiya ya Kikristo Tanzania ambayo yanaratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii [CSSC]
………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu katibu mkuu Elimu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa[TAMISEMI] Bw.Gerald  Mweli kupitia mwakilishi wake kaimu Mkurugenzi wa Elimu na Utawala Dkt. George Jidamva ametoa Rai kwa Taasisi za dini za Elimu hapa nchini kuhakikisha  zinaitumia vyema Tume(cssc), ili liwe Daraja imara la kuwasilisha hoja serikalini.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa wakuu wa shule za sekondari za Makanisa nchini yanayoratibiwa na Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii[CSSC]  ,kwa niaba  ya Naibu Katibu mkuu TAMISEMI- Elimu,kaimu mkurungezi wa elimu na utawala Dkt.George Jidamva amesema Tume ya kikristo ya huduma za jamii[CSSC] imekuwa na Mchango mkubwa katika  jamii hivyo ni vyema ikaungwa mkono kwa jitihada zote  za kusimamia ubora wa elimu nchini kwa makanisa

“Ni jambo jema kwamba wazazi wengi wanafurahishwa  na juhudi za Makanisa katika utoaji wa elimu nchini,ni imani yangu mtaendelea kutoa elimu iliyobora  na Maadili mema  kwa kufuata taratibu,sera,sheria na miongozo iliyopo hivyo tume ya CSSC imekuwa ikifanya kazi kwa uwazi, na nitoe rai tu kwa Taasisi za Makanisa kuitumia vyema ili liwe daraja imara  la kuwasilisha hoja kwa serikali”amesema.

Aidha ,ametumia Fursa hiyo kuipongeza TUME ya kikristo ya huduma za jamii( CSSC ) kwa kuanzisha   Huduma ya udhibiti ubora  ,uhakiki wa Takwimu na Mitihani ya pamoja  kwa Madarasa ya Mitihani kitaifa  huku akiasa kuweka Mazingira Mazuri ya Ushirikiano   kwa ngazi ya kata na Halmashauri.

Katika hatua nyingine , amesgauri ombi la asilimia moja ya gharama za uendeshaji wa shule [WCF] kufanana na ya serikali ya asilimia 0.5 iletwa kwa maandishi yenye ufafanuzi na Tume kwa hatua zaidi.

Mkurugenzi wa Elimu wa Tume Kikristo  ya Huduma za jamii[CSSC]Mwalimu Petro Masatu Pamba amesema ufaulu kwa shule za makanisa umekuwa chachu nchini ambapo mwaka 2013 hadi 2018  matokeo ya kidato cha nne kwa shule zilizo na wanafunzi zaidi ya 40 ,shule 100 bora  ,kanisa limekuwa  na ufaulu wa wastani wa asilimia 70%.

Pia amesema Makanisa yameendelea kuboresha ufundishaji wa Masomo ya sayansi kwa kutumia TEHAMA.

“shule 42 mpaka sasa zinatumia mfumo huu kwa uratibu wa PLATFORM ya Tume.

Walimu,wanafunzi na Menejimenti ya Shule kuboresha umahiri kwa wanafunzi  na matumizi ya utawala”amesema.


Akitoa neno la Shukrani, Padri kutoka jimbo katoriki la Moshi mkoani Kilimanjaro ,Padri.William  Ruwahi’ch ameipongeza Serikali kwa kuendelea kushirikiana na Taasisi za dini .

”Tunashukuru sana kwa serikali kwa kuendelea kuthamini mchango wa  shule za kanisa ,tunaahidi kuhakikisha tunatoa elimu bora”amesema.

Aidha,amesema kuna changamoto kubwa ikiwa ni pamoja na leseni ya Biashara kwani taasisi za kanisa zinatoa huduma na si za kibiashara.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com