Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameiagiza Bodi na Watendaji
wa SACCOS kuwasilisha Rasimu za Taarifa za Fedha kwa Wakaguzi wa Nje (COASCO)
kabla au ifikapo tarehe 31.01.2020.
MHandisi
Mtigumwe ametoa agizo hilo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa ni lazima
kuwasilisha mapema taarifa hizo ili Ukaguzi uweze kufanyika kwa wakati na
Taarifa za Ukaguzi ziwasilishwe kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliopangwa
Kisheria.
Amewataka
wanachama wote wa SACCOS hususani Bodi na Watendaji wa SACCOS nchini kuwa,
matakwa ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018 (The Microfinance Act
2018), kuhusu ukaguzi wa nje hivyo ni lazima kutekeleza agizo hilo kwa wakati.
“SACCOS zote zinatakiwa kuhakikisha kuwa Taarifa za Fedha
za Mwaka 2019 ziwe zimekaguliwa na kuwasilishwa Benki Kuu au kwa Mamlaka
iliyokasimiwa ambayo ni Mrajis wa Vyama Vya Ushirika ifikapo tarehe 30 Aprili,
2020” Alisema
MWISHO
Safi .
ReplyDelete