Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua shamba la mifugo mara baada ya kutembelea Chuo cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya, tarehe 21 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya, tarehe 21 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua maabara ya udongo mara baada ya kutembelea Chuo cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya, tarehe 21 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Uongozi na wanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya, tarehe 21 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua eneo linalozalisha miche ya mikorosho mara baada ya kutembelea Chuo cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani Mbeya, tarehe 21 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya
Serikali imeeleza dhamira yake ya
kukarabati vyuo vyote vya kilimo nchini ili kukabiliana na changamoto
zinazovikabili vyuo hivyo ambapo ni pamoja na uchache na uchakavu wa vitendea
kazi kama maabara, vifaa vya TEHAMA, na zana za kilimo yakiwemo matrekta.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet
Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 21 Disemba 2019 wakati alipotembelea Chuo
cha Kilimo cha Uyole (MATI Uyole) wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya siku
tatu mkoani Mbeya.
Ameeleza kuwa dhamira ya kukarabati
vyuo hivyo imetokana na kujionea uchakavu wa miundombinu ikiwemo barabara, mifumo
ya maji, majengo (Mabweni na nyumba za watumishi) katika chuo hicho pamoja na
vyuo vingine vya kilimo.
Amesema kuwa serikali itakarabati
vyuo hivyo ili kuwa na vyuo vya kisasa vinavyopendeza na vitakavyokuwa chachu
ya kupata wataalamu waliokomaa kupitia mitaala iliyoboreshwa na zana bora za
kilimo.
Pia, Mhe Hasunga amesema kuwa ili
kuwa na wataalamu waliobobea vizuri kwenye sekta ya kilimo wizara yake
imekusudia kuongeza muda wa mafunzo kwa vitendo (Field) kufikia mwaka mmoja kwani
kufanya hivyo kutaongeza msukumo na kumjengea uwezo mkubwa mwanafunzi.
“Tutafanya hivyo ili kuona
alichojifunza mwanafunzi kama kina akisi weledi katika jamii na kama wazo hilo likikubalika
tutarekebisha mitaala yetu ya kufundishia katika vyuo vyote vya kilimo na vyuo
vikuu” Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika, Waziri
Hasunga amewaagiza wakufunzi wa chuo cha kilimo cha Uyole (MATI Uyole)
kuhakikisha kuwa wanaandika vitabu na majarida mbalimbali kwani maarifa na
ujuzi walionao utasaidia kuhakikisha kuwa kile walichonacho kinawafikia watu
wengi zaidi.
Amesema kuwa
machapisho na vitabu watakavyoandika vitasaidia katika siku za usoni wanafunzi
kuweza kujifunza na kuona umuhimu wa kuandika vitabu ama majarida.
Waziri Hasunga
ameongeza kuwa wizara ya kilimo inaendelea kufanya Mabadiliko ya kisera na
kisheria ili kuimarisha sekta ya kilimo na wakulima nchini kuondokana na dhana
ya kilimo cha kujikimu na kuwa na kilimo cha kibiashara.
Ameongeza kuwa dhamira
kubwa kabisa ni pamoja na kuwa na kilimo chenye uwezo wa kutoa ajira na mchango
mkubwa katika sekta ya viwanda na kuongeza fedha za kigeni.
“Sasa ili kufikia
kilimo cha namna hiyo kuwa na utitiri wa Bodi inaonekana usimamizi wake kupwaya
hivyo tunakusudia katika mabadiliko hayo kuziunganisha bodi zote na kuwa na
Bodi tatu pekee” Alisema
Waziri Hasunga
ameongeza kuwa tayari kamati maalumu ya wataalamu imetuama Jijini Dodoma ili
kutathmini vyuo 14 vya kilimo vilivyopo, vituo 17 vya utafiti na vingine vidogo
23 ili kubaini kiasi mahususi kinachohitajika ili kufanya maboresho ya vyuo
hivyo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment