Diwani wa Kata ya Sinde Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe
akizungumza mbele ya waumini wakati wa ibada ya Mwaka Mpya iliyofanyika katika
kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry)
lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya, Jana Januari
Mosi, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza
waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T.
Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana
na Diwani wa Kata ya Sinde Mkoani Mbeya Mhe Newton Mwakijobe wakati wa ibada ya
Mwaka Mpya iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus
Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga
Jijini Mbeya, Jana Januari Mosi, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza
waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T.
Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiongoza
waumini wa kanisa La Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre T.
Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde B, Kata ya Manga Jijini Mbeya
kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
na serikali yake wakati wa ibada ya Mwaka Mpya, 2017.
Na Mathias Canal,
Mbeya
Diwani wa Kata ya Manda Wilaya na Mkoa wa Mbeya Mhe Newton
Mwakijobe amesifu Utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwatetea
wanyonge huku akisimamia nidhamu na uwajibikaji kazini.
Diwani Huyo ametoa pongezi hizo wakati akitoa salamu wakati wa
ibada ya Mwaka Mpya iliyofanyika katika kanisa La Huduma ya Maombezi na
Uponyaji (Jesus Healing Centre T. Ministry) lililopo Katika Mtaa wa Sinde
B, Kata ya Manga Jijini Mbeya.
Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, Diwani Huyo amesifu zaidi usimamizi madhubuti wa
rasilimali za Taifa unaofanywa na Rais Magufuli ambao utawanufaisha wananchi
wote si MTU mmoja mmoja.
Mhe Mwakijobe pia amempongeza Rais Magufuli kwa kumchagua Mhe
Mwanjelwa katika serikali yake kuwa Naibu Waziri anayeshughulikia sekta ya
Kilimo jambo ambalo limeonyesha chachu na hamasa ya kuwakumbuka wakazi wa Mbeya
Mjini kwa kupata Waziri wa kwanza tangu nchi ilipopata Uhuru.
Aidha, Mhe Mwakijobe alimsihi Mhe Mwanjelwa kumfikishia salamu
Rais Magufuli ikiwa ni pamoja na kumuomba kuzuru Mkoani Mbeya katika ziara yake
ya kikazi ili kuzungumza na wananchi wa Mkoa wa Mbeya ambao wanatambua majukumu
makubwa na mazito anayoyafanya kwa manufaa ya wananchi wote.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo aliongoza
waumini wa kanisa la Huduma ya Maombezi na Uponyaji (Jesus Healing Centre
T. Ministry) kumuombea Rais Magufuli sambamba na serikali kwa ujumla ili
wananchi waendelea kujivunia matunda ya kiongozi Huyo makini na shupavu.
Mhe
Mwanjelwa Alisema kuwa maombi hayo ni kwa ajili ya kumshukuru Mungu, kwa
kuwawezesha kumpata Rais John Magufuli, ambaye amekuwa akiibua na kufichua
maovu mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka nchini.
Aliongeza
kuwa, juhudi alizozionyesha Mhe Rais Magufuli zinafaa kuungwa mkono na jamii
yenye hofu na Mungu kwani ndani yake kuna mtihani mgumu unaohitaji kumuweka
kwenye maombi ya wananchi ya kila siku katika sehemu yeyote iwe kazi na hata
majumbani.
Kanisa hilo pia limefanya ibada maalumu kwa ajili ya Mhe
Mwanjelwa ili awe kiongozi shupavu mwenye maono na utendaji uliotukuka katika
serikali na aweze kuwa muwakilishi mzuri wa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Taifa
kwa Ujumla wake.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment