Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Katikati) akimkabidhi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto), akisisitiza jambo wakati wa makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo wakifatilia mkutano huo.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga Katikati) akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati wa hafla ya makabidhiano ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kwa TAKUKURU hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma. Mwingine pichani ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbung’o.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Katika mwaka wa fedha wa 2018/19 Serikali
ilitoa maagizo kwa Shirika la COASCO kukagua Vyama vya Ushirika vyote. Mpaka
tarehe 30 Juni, 2019 Vyama vya Ushirika vilivyosajiliwa vilikuwa 11,410. Kati
ya Vyama hivyo, Vyama hai ni 6,463; Vyama Sinzia ni 2,844 na Vyama ambavyo
havipatikani 2,103.
Kutokana na maagizo hayo, hadi kufikia tarehe
30 Juni, 2019 COASCO ilikagua Vyama vya Ushirika vipatavyo 4,413 sawa na
asilimia 102.63 ya Lengo la Serikali la kukagua Vyama 4,300.
Katika vyama hivyo 4,413 vilivyokaguliwa,
vyama 303 (6.87%) vilipata Hati inayoridhisha, vyama 2,378 (53.89%) vilipata
Hati yenye shaka, vyama 879 (19.92%) vilipata Hati isiyoridhisha na vyama 853
(19.32%) vilipata Hati mbaya.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ametoa
takwimu hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kumkabidhi
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Brigedia Jenerali John Mbung’o ya muhtasari wa uchambuzi wa ukaguzi wa vyama
vya Ushirika uliofanywa na Shirika la Ukaguzi wa Vyama vya Ushirika COASCO
katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Wizara ya Kilimo katika mji wa serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Waziri Hasunga alisema
kuwa Kati ya Vyama Vikuu 38,Vyama 4 vilipata Hati Safi, vyama 22 vilipata Hati
yenye shaka, 9 vilipata hati isiyoridhisha na 3 hati mbaya. Vyama hivyo Vikuu 3
vilivyopata HATI MBAYA inayohusisha hoja zenye viashiria vya ubadhirifu wenye
Jumla ya shillingi 856,357,955 kwa RUNALI, SCCULT 4,878,662,431 na KYECU kwa
kukosekana kwa hati za kuhesabu mali za kudumu mwisho wa mwaka.
Alisema kuwa Chama Kilele
(Shirikisho-TFC) kimepata Hati Isiyoridhisha ambayo inajumuisha fedha benki
zisizofanyiwa malinganisho na pia kutooneshwa katika taarifa za fedha kiasi cha
shilling 1,538,726,787
Kati ya Vyama vya
Ushirika wa Mazao (AMCOS) 2,710
vilivyokaguliwa, vyama 15 vilipata Hati Safi, 1347 Hati yenye Shaka, 599 Hati
Isiyoridhisha na vyama 749 vilipata Hati Mbaya.
Matatizo makuu katika vyama hivyo vya AMCOS ni kushindwa kuandika vitabu
vya hesabu, malipo mengi kutokuwa na vielelezo vya malipo, mifumo dhaifu ya
udhibiti wa makusanyo na mauzo ya mazao, kukosekana kwa daftari la mali za
vyama na watendaji wa vyama kutokuwa na weledi wa kuandika vitabu na taarifa za
fedha za vyama. Kati ya SACCOS 1,448 SACCOS 261 zilipata Hati Safi, 887 yenye
Shaka, 218 Isiyoridhisha na 82 Hati Mbaya.
Waziri wa Kilimo Mhe
Japhet Hasunga ameyataja matatizo makuu ya SACCOS nyingi kuwa ni kushindwa
kuandika vitabu ipasavyo, marejesho ya mikopo ya wanachama kutofanyika kwa
wakati, baadhi ya waajiri kuchelewesha kuwasilisha makato ya wanachama kwa
SACCOS, madeni makubwa yanayothiri utendaji wa SACCOS, miamala ya benki
kutofanyiwa malinganisho na baadhi ya miamala kuwa na ubadhirifu.
Mhe Hasunga amesema kuwa katika ukaguzi wa
kawaida kwa mwaka 2018/2019 Fedha zenye
Mashaka (nia ovu) ni Tsh 87,694,976,970, Hasara
iliyotengenzwa kwa uzembe ni Tsh 22,861,038,064 huku Wizi/Ubadhirifu
ikiwa ni Tsh 2,840,752,866 ambapo jumla ya fedha hizo ni Tsh 113,396,767,900
Pia
alisema kuwa katika ukaguzi maalumu kwa mwaka huo wa 2018/2019 Fedha zenye Mashaka (nia ovu) ni Tsh 6,266,796,345.63, Hasara iliyotengenzwa kwa uzembe ni
Tsh 2,634,438,512.00 wakati Wizi/Ubadhirifu
ni Tsh 1,755,248,116.00 ambapo jumla yake ni Tsh 10,656,482,973.63
Amesema kuwa jumla kuu ya fedha za
ukaguzi wa kawaida na ukaguzi maalumu ni kwa mwaka wa fedha 2018/2019 mi Tsh 124,053,250,874.00
Alisema kuwa mbali na
vyama hivyo vilivyokaguliwa, vipo vyama 682 vilikataa kuwasilisha vitabu kwa
ajili ya ukaguzi na kuongeza kuwa Kati ya vyama 853 vyenye Hati Mbaya, vipo
vyama vyenye viashiria vya ubadhirifu wa fedha na mali vipatavyo 130 na vyama
vyenye matatizo mbalimbali ya uongozi na utendaji 723.
Pia, Amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa hiyo
aliyoikabidhi TAKUKURU baadhi ya Waajiri wameonekana kuchelewesha michango ya Wanachama
baada ya makato na kuathiri uhai wa vyama katika kutoa mikopo kwa Wanachama.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment