Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi (hawapo
pichani) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hospitali
ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimpongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuweka jiwe
la msingi katika ujenzi wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa wilayani
Chamwino, Dodoma.
Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino, Dodoma.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitizama ramani ya
mchoro sanifu wa kengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani
Chamwino, Dodoma.
Picha ya Mchoro sanifu wa jengo la Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
Umati wa wananchi waliojitokeza
kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa
Hospitali ya Uhuru inayojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma.
***********************************
Na Englibert Kayombo, WAMJW – Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa Serikali
inayo fedha za kutosha kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya
Uhuru.
Rais Magufuli amesema hayo leo alipokuwa akizungumza
na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa hospitali hiyo inayojengwa wilayani Chamwino,
Dodoma.
“Fedha ya ujenzi wa hospitali ipo, tunayo Billioni 3.4”
amesema Rais Magufuli ambaye ameonyesha
kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Rais Magufuli amesema kuwa mwanzoni TBA ilipewa kazi
ya ujenzi wa hospitali hiyo lakini hawakusimamia vizuri
ujenzi kupelea Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI
Mhe. Seleman Jafo kuchukua maamuzi ya kukabidhi kazi
kwa Jeshi la Kujenga Taifa ili kazi hiyo ikamilike kwa
wakati.
Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenarali
Charles Mbuge aliyepewa jukumu la kusimamia ujenzi wa
Hospitali hiyo amesema kuwa Jeshi lake linauwezo wa
kufanya kazi hiyo na kuikamilisha ndani ya muda
uliopangwa.
“Mheshimiwa Amiri Jeshi Mkuu, Jeshi letu lina nguvu ya
kutosha na tutamaliza kwa muda kazi hii, sina mipango
mingine ni kumaliza tuu” amesema Brigedia Jenerali
Mbuge.
Mnamo tarehe 9 Desemba, 2018, Rais Magufuli alitoa
maagizo ya fedha zilizotengwa kugharamia sherehe za
uhuru kiasi cha Shilingi Milioni 995 kutumika kujenga
hospitali katika Mkoa wa Dodoma. Kukamilika kwa
hopitali hiyo kutatatua kero waliyokuwa wanaipata
wananchi ya umbali wa kufuata huduma za afya.
0 comments:
Post a Comment