Na Mwandishi Wetu-WAMJW
Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa pole kwa Anna Zambi mwenye
umri wa miaka 16, ambaye amefiwa na wazazi wake wote wawili pamoja na
ndugu zake watatu.
Waziri Ummy ameyasema hayo kupitia
ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Serikali kupitia
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipo tayari
kutoa msaada wa kisaikolojia.
“Pole nyingi kwa binti yetu Anna
Zambi, hili jambo ni kubwa mno kwa huyu mtoto, inaumiza sana,
ninamwombea kwa Mungu ampe nguvu na moyo wa uvumilivu katika kipindi
hiki kigumu,nasi Wizara tukiwa na jukumu na dhamana ya kusimamia ustawi
na maendeleo ya watoto nchini tunachukua jukumu la kuratibu na kusimamia
psychosocial support ya mtoto huyu pamoja na masuala mengine yanayohusu
ustawi wake kwa ujumal” alizema Waziri Ummy.
Waziri Ummy alimuagiza Katibu Mkuu
Idara Kuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu
kuratibu masuala ya utoaji wa huduma ya kisaikolojia kwa Mtoto Anna na
Katibu Mkuu huyo amemtembela mtoto Anna nyumbani kwao Goba jijini Dar es
Salaam na kutoa salamu za polekwa niaba ya Wizara.
Akizungumza mara baada ya kutoa
salamu za pole Dkt. John Jingu amesema kuwa Wizara imeshatoa Maafisa wa
Ustawi wa Jamii kuanza kutoa huduma ya msaada wa kisaikolojia kwa Mtoto
Anna na kuuhakikisha kuwa Serikali itamsaidia Mtoto huyo ili aweze
kurudi katika hali yake ya kawaida.
Ameongeza kuwa Serikali itakuwa
bega kwa bega na familia katika kuhakikisha mirathi inasimamiwa vizuri
ili aweze kupata haki zake zote bila kuingiliwa na mtu yoyote kwani ni
yupo katika wakati mgumu sana kwa kuondokewa na familia yake yote.
“Nikuhakikishie tutasimamia na
utapata msaada mzuri na tunaamini utakaa sawa na tunakuombea kwa
Mwenyezi Mungu akuoe nguvu na faraja katika kipindi hiki kugumu
unachopitia tuko pamoja na wewe” alisema Dkt. Jingu
Wazazi wa Anna- Lingston Zambi na
Winfrida Lyimo pamoja na ndugu zake watatu Lulu, Adrew na Grace
walifariki Dunia Oktoba 26 mwaka huu wakiwa njiani kutoka jijini Dar es
Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro, kwenye mahafali ya Kidato cha Nne ya
Anna, ambapo gari waliokua wakisafiria lilisombwa na maji na mafuriko
yaliyotokea wilayani Handeni mkoani Tanga.
0 comments:
Post a Comment