NA Khalfan Said, Mtwara
WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa amezindua
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG) katika Kongamano la Uwekezaji
na
Maonyesho ya Biashara lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara.
Maonyesho ya Biashara lililofanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara.
Mwongozo
huo umetayarishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
kwa kushirikiana na Mkoa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa
Mataifa (UNDP).
Mataifa (UNDP).
“Kuja
kwenu Mtwara leo hii hamjapoteza nauli na muda wenu, mmekuja Mtwara
mahali sahihi kwa uwekezaji na mtatumia nafasi ya leo kusikia nini
kimeandaliwa kwa
ajili ya kuwaambia fursa zipi zinapatikana mkoani Mtwara.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
ajili ya kuwaambia fursa zipi zinapatikana mkoani Mtwara.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ya awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kuiondoa
Tanzania kwenye uchumi wa chini kwenda Uchumi wa Kati na hakuna njia
nyingine isipokuwa ni kuvutia uwekezaji, Serikali inakaribisha
wawekezaji kuwekeza hapa nchini iwe ni Mtanzania au mgeni kutoka nje ya
nchi atapokelewa ili aweze kuwekeza hapa
nchini.
nchini.
“Wakati
nikizungumza na wakuu wa mikoa Juni 18, 2018 jijini Dodoma nilitoa
maelekezo na dira ya kila mkoa kupata wawekezaji, niliagiza kila mkoa
lazima ujipange kuhakikisha unatangaza fursa zilizopo katika mkoa.” Alifafanua Waziri Mkuu.
Mheshimiwa
Majaliwa alisisitiza Mikoa ambayo bado haijaandaa miongozo ya uwekezaji
ifanye hivyo mara moja kabla mwaka huu haujaisha. Pia aliwaonya
watumishi wanaokuwa vikwazo kwa wawekezaji waache mara moja na
wanaobainika wachukuliwe hatua stahiki.
“Niipongeze
Taasisi ya ESRF chini ya Mkurugenzi wake Dkt. Tausi Kida imefanya kazi
kubwa na nzuri, baada ya kufanya utafiti imetoa tathmini ya nini
kifanyike, wapi tufanye
nini ili tuweze kufanikisha uwekezaji hapa nchini” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa na kuongeza….Kila ninapokwenda kuzindua Miongozo ya Uwekezaji nimekuwa nikukutana na ESRF ikiongozwa na Dkt. Tausi Kida, hongera sana kwa kazi nzuri mnayofanya.” Alipongeza Waziri Mkuu.

Mkuu pia ameipongeza UNDP kwa kufanya kazi kwa pamoja na Serikali na
kuahidi kuwa Serikali itaunga mkono shughuli za UNDP ambazo Serikali ya
awamu ya Tano
na zile zilizotangulia daima zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na UNDP na zinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kimataifa.
na zile zilizotangulia daima zimekuwa zikifanya kazi kwa pamoja na UNDP na zinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hii ya kimataifa.
Uzinduzi
huo pia ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki. Wakati akimkaribisha
Waziri Mkuu kuhutubia,
Mhe. Kairuki alieleza hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kupelekea Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 144 hadi 141 kwenye urahisi wa kufanya biashara duniani.
Mhe. Kairuki alieleza hatua ambazo Serikali imechukua kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kupelekea Tanzania kupanda kutoka nafasi ya 144 hadi 141 kwenye urahisi wa kufanya biashara duniani.
Mawaziri
wengine waliohudguria na kutoa neno ni Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhe. Innocent Bashungwa, na Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga.
Wakati
akitoa salaamu, Mwenyeji wa Mkoa huo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius
Byakanwa aliwakaribisha wageni waalikwa na kuelezea jinsi Mkoa
ulivyojipanga kuwapokea
na kuwasaidia wawekezaji. Pia alitoa fursa kwa Wakuu wa Mikoa jirani walihudhuria halfla hiyo ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mtwara
kutoa neno. Waliohudhuria ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Chrintina Mdema na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo.

Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi.Christine
Musisi alisema UNDP itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika
kuboresha maisha ya wananchi. Alisema UNDP itaendelea kusaidiana na
Mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kutoa ushauri wa kitaalam
na rasilimali fedha panapohitajika.
Awali
akiwasilisha Muhtasari wa Fursa za Uwekezaji katika Mkoa wa Mtwara
katika Kongamano la Uwekezaji, Mtafiti Mkuu Mshiriki kutoka Taasisi ya
Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF) Dkt. Oswald Mashindano alisema ESRF ilifanya utafiti kwenye halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara na utafiti huo ulibaini uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji. Dkt. Mashindano alitaja timu ya wataalam kutoka ESRF walioshiriki kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji ikijumuisha Prof. Haidari Amani, Bi. Margareth Nzuki, Bw. Mussa Mayala Martine, na Bw. James Kasindi.

Dkt.
Mashindano alitaja fursa mbalimbali za uwekezaji ambazo zimepewa
kipaumbele na mkoa. Fursa hizi ziko katika makundi mbalimbali ikiwa ni
pamoja na uwekezaaji
katika kilimo hasa korosho, kilimo cha umwagiliaji wa mpunga na miwa, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na mazao ya bustani; uwekezaji katika
mifugo hasa ranchi na unenepeshaji wa mifugo; uwekezaji katika uvuvi hasa uvuvi
ndani ya bahari kwa kutumia nyenzo na teknolojia za kisasa pamoja na ufugaji wa
samaki; uwekezaji katika viwanda hasa Kuchakata Korosho na mazao mengine kama
mhogo, nazi, choroko, mbogamboga na matnda, kuchakata na kufungasha chimvi,
Chakula cha Mifugo, Kuchakata Samaki, Kiwanda cha Kutengeneza Maji ya Chupa nk.

Fursa
za uwekezaji katika eneo la miundombinu zilijumuisha ujenzi wa jengo kwa ajili
ya matengenezo na maegesho ya ndege, stendi za kisasa, ujenzi wa kituo cha
michezo ikijumuisha uwanja wa mpira, masoko ya kisasa nk. Aidha Dkt. Mashindano
alitaja makundi mengine ya fursa za uwekezaji kuwa ni pamoja na uwekezaji
katika utalii akilenga uwekezaji kwenye fukwe, michezo ya baharini, ujenzi wa
hoteli, majumba ya starehe, kambi za watalii, kuendeleza maeneo ya kihistoria
nk. Pia zilibainishwa fursa za uwekezaji katika huduma za kijamii zikijumuisha
afya na elimu. Kwa upande wa afya kuna fursa ya ujenzi wa hospitali na kiwanda
cha kutengeneza maji ya wagonjwa na vifaa tiba. Kwa upande wa elimu alitaha
fursa ya kuendesha chuo maalum cha ujuzi pamoja na shule binafsi za kisasa.

Baada
ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji washiriki walipata fursa ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya uwekezaji Mkoani Mtwara.
ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji washiriki walipata fursa ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya uwekezaji Mkoani Mtwara.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (watatu kushoto), akikata utepe, kuzindua
Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa wa Mtwara (MIG), kwenye Chuo Cha Ualimu
Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni kutoka kulia ni Waziri wa
Kilimo Mhe. Japhet Hasunga, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Bi. Christine Msisi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Gelasius Byakanwa.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), akionyesha nakala za Mwongozo wa
Uwekezaji Mkoani Mtwara (MIG), baada ya kuuzindua kwenye Chuo Cha Ualimu
Mtwara Novemba 1, 2019. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia), Mwakilishi Mkazi
wa UNDP, Bi. Christine Msisi (wapili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mhe.Gelasius Byakanwa (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF,
Dkt. Tausi Kida.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida, huku Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angela Kairuki (katikati)
akishuhudia, mara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara Novemba 1, 2019.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia kongamano hilo na kisha kuzindua Mwongozo huo Novemba 1, 2019.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine
Msisi akitoa hotuba yake.
Viongozi waandamizi wa ESRF walioshiriki katika utafiti huo kutoka kushoto,Bw. Mussa Mayala Martine, Dkt. Oswald Mashindano na Bi.
Margareth Nzuki.
Margareth Nzuki.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga huku Mhe.
Kairuki (katikati) akishuhudia.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG), Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa huku Mhe. Kairuki (katikati) akishuhudia.
Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akimpatia nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji
Mkoa wa Mtwara (MIG) Mwakilishi Mkazi wa UNDP hapa nchini, Bi. Christine
Msisi. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji), Mhe. Angela Kairuki (wapili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji
wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida. Mwongozo
huo umetayarishwa na (ESRF) kwa
kushirikiana na Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
huo umetayarishwa na (ESRF) kwa
kushirikiana na Mkoa wa Mtwara chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP).
0 comments:
Post a Comment