Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson
alikuwa Mgeni rasmi katika Tamasha la kuimarisha Jumuiya ya Umoja wa
Vijana wa CCM mkoa wa Mbeya lililofanyika katika viwanja vya Sokoine
ambapo kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa michango mbalimbali
kwa makundi tofauti yalishoshiriki katika tamasha hilo.
Miongoni mwa michango hiyo ni
pamoja na kituo cha Afya cha Makongolosi Chunya ambacho kimepata
Shilingi Milion tano (Tsh 5,000,000/-), Umoja wa Wanawake Tanzania mkoa
wa Mbeya waliopewa Computer mpakato yenye thamani ya Milion mbili (Tsh
2,000,000/-), Umoja wa vijana CCM mkoa wa Mbeya waliopewa Pikipiki moja
yenye thamani ya shilingi Milion mbili na laki mbili (Tsh 2,200,000/-),
Murua Group wamepewa Milion mbili (Tsh 2,000,000/-) pamoja na Umoja wa
Machifu Igawilo waliopewa jumla ya shilingi Milion moja (Tsh
1,000,000/-) ambapo jumla ya Shilingi Milion kumi na mbili na laki mbili
zimetolewa zimetolewa na taasisi hiyo ili kuwawezesha kuendesha
shughuli zao kwa ufanisi.
Katika hotuba yake Dkt. Tulia
amesema “Kama mnavyofahamu kwamba mimi sio Mbunge wa sehemu moja hivyo
basi hata kwenye Wilaya nyingine huko tumekwishafanya wote kazi na
tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuimarisha chama chetu lakini
kwa leo wenyeji wetu walikuwa ni Mbeya jiji na lazima jumuiya zetu
zifanye kazi vizuri na kwa ufanisi.”
0 comments:
Post a Comment