Mbunge wa Geita mjini ambaye pia
ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu
akizungumza na wananchi wa eneo la Mpomvu katika kata ya Mtakuja wakati
akiwatambulisha Wenyeviti wateule wa CCM.
Katibu wa Mbunge wa Geita mjini,
Mariamu Mkaka akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa kuwatambulisha
Wenyeviti wateule wa Serikali za mitaa wa CCM katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika eneo la Mpomvu kata ya Mtakuja mkiani Geita.
Msanii wa Vichekesho maarufu kwa
jina la Kigwendu Kingwendulile akiwaburudisha wananchi waliofika ktika
eneo la Mpomvu kwa ajili ya kuwatambulisha wakazi wa eneo la Mpomvu
kabka ya Mbunge wa Geita mjini kuzungumza nao.
Mwenyekiti wa Mtaa
wa Benue, James Manakila akiwatambulisha Wajumbe wa mtaa wake kwa Mbunge
wa Geita mjini Mhe.Constantine Kanyasu.
*****************************
Mbunge wa Geita mjini
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameanza
kuwatambulisha Wenyeviti wateule wa Chama cha Mapinduzi( CCM) kwa
wananchi kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa
kufanyika mwishoni mwa wiki hii.
Akizungumza na
Wananchi wa eneo la Mpomvu katika Kata ya Mtakuja mkoani Geita,
Mhe.Kanyasu ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio yaliyopatikana katika
katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka minne.
Katika mkutano huo,
Mhe.Kanyasu amewatambulisha Wenyeviti wateule wa mitaa saba kwa wananchi
na kuwataka watoe ushirikiano ili kuleta maendeleo.
Ametaja mafanikio hayo kuwa yamepatikana katika nyanja ya Elimu, Afya, Barabara, mikopo pamoja na Umeme.
Mbali ya kuelezea
mafanikio hayo yaliyopatikana katika utekezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
CCM (2015-2020) katika jimbo hilo, Mhe.Kanyasu ametaka wananchi kutoa
ushirikiano kwa Wenyeviti wapya watakaopatikana katika uchaguzi huo ili
kuharakisha miradi ya maendeleo.
0 comments:
Post a Comment