Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella
Ikupa,akisalimiana na Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe. Kenneth Yindi
alipowasili kwa ajili ya kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu wenye
ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino iliyopo jijini
Dodoma
Mkurugenzi wa NAKUA NA TAIFA
LANGU, Jessica Mshama,akitoa taarifa wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali
kwa watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino
iliyopo jijini Dodoma
Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe.
Kenneth Yindi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Ujasiriamali kwa
watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino iliyopo
jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella
Ikupa,akizungumza na watu wenye ulemavu wakati kufunga mafunzo ya
Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya
Chamwino iliyopo jijini Dodoma
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella
Ikupa,akiwatunuku vyetu baadhi ya wajasiriamali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella
Ikupa,akikata utepe kuashiria kufunga wa mafunzo ya Ujasiriamali kwa
watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri Wilaya ya Chamwino iliyopo
jijini Dodoma.
…………………………….
Na.Alex Sonna,Chamwino
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe Stella
Ikupa,amesema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau katika
kutoa elimu kwa watu wenye uhitaji maalum ili kuweza kuwanasua katika
kundi la ombaomba na kuwafanya wawe tegemezi kwa kuwa na miradi yenye
kuwapa kipato.
Kauli hiyo ametoa wakati akifunga
mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu wenye ulemavu katika Kata ya Buigiri
Wilaya ya Chamwino iliyopo jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yalianza toka Novemba
29 ambapo yaliandaliwa na Taasisi ya NAKUA NA TAIFA LANGU kwa
kushirikiana na Diwani wa Kata hiyo Mhe Kenneth Yindi ambapo yalihusisha
watu wenye ulemavu na wanawake.
Elimu iliyotolewa ni Elimu ya
kujitambua, Elimu ya usindikaji bidhaa kwa vitendo, Elimu ya masoko,
Athari ya matumizi ya rushwa katika upatikanaji wa huduma, Umuhimu na
utaratibu wa kuunda vikundi vya walemavu na wanawake pamoja na Elimu ya
matumizi sahihi ya fedha za mikopo.
Mhe. Ikupa amempongeza Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo ya NAKUA NA TAIFA LANGU, Jessica Mshama kwa uzalendo
alionao kwa kuamua kutoa elimu kwa watanzania wenzake ambayo itawaondoa
kwenye lindi la umaskini.
” Nikupongeze sana Jessica
umefanya jambo kubwa siyo tu kwa Wananchi wa Buigiri bali kwa Taifa lako
kwa ujumla. Elimu hii uliyowapa ina manufaa makubwa kwao wenyewe na
hata kwa kizazi chao. Niwaahidi Serikali itaendelea kushirikiana na
wadau wote wa maendeleo katika kuwakomboa watu wetu,” Amesema Mhe Ikupa.
Amesema ili kufikia uchumi wa kati
kupitia viwanda ni lazima kila kundi nchini lihusike katika uzalishaji
na kuwapongeza wahitimu hao kwa kuelewa mafunzo vizuri na kuanza
kutengeneza bidhaa zao ikiwemo Ubuyu, Siagi ya Karanga pamoja na Sabuni.
Awali Mkurugenzi wa NAKUA NA TAIFA
LANGU, Jessica Mshama amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu ya
kujitegemea watu wenye ulemavu ili kuepukana na dhana ya kwamba walemavu
wote ni ombaomba.
Amesema Serikali ya awamu ya tano
imepiga hatua kwenye maendeleo hivyo wao kama wadau wana kila sababu ya
kusaidia Rais Magufuli katika kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
” Mhe Waziri tunashukuru kwa
kufungua na kufunga mafunzo haya. Tunakuahidi kuwa Taasisi yetu
itaendelea kutoa mafunzo haya Nchi nzima lakini pia kuwatafutia masoko
ya bidhaa wanazotengeneza hawa wahitimu.
Tayari Dodoma tushatoa elimu kwa
watu 300 hapa Chamwino na Wilaya ya Chemba, tutaenda Kongwa, Mpwapwa na
Wilaya zingine. Lakini lengo letu ni kuona tunawainua kiuchumi walemavu
na wanawake nchini,” Amesema Jessica.
Kwa upande wake Diwani wa Kata
hiyo, Kenneth Yindi ameishukuru Serikali na Taasisi hiyo kwa kutoa
mafunzo hayo ambayo anaamini yataenda kubadilisha mtazamo na fikra za
wananchi wa Kata ya Buigiri.
Amesema mafunzo hayo yamewasaidia
kuweza kujitambua na kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zitakua na
nembo ya Buigiri jambo ambalo litasaidia Kata yao kukua kimaendeleo na
kuvutia watu kuja kuwekeza na hivyo kuongeza mapato ndani ya Halmashauri
yao.
” Hakika tunaipongeza Taasisi ya
NAKUA NA TAIFA LANGU kwa kuendesha mafunzo haya, wametoa kiasi cha Sh
Milioni Tatu za ueneshaji sambamba na walimu wawili, huu ni uzalendo
mkubwa waliouonesha kwetu na tuwaombe waendelee kushirikiana na Serikali
yetu ili kufikia kundi kubwa la watu wenye uhitaji,” Amesema Yindi.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo,
John Masaka ameishukuru Serikali kwa kuendelea kushirikiana na wadau wa
Maendeleo katika kufanikisha inawakomboa wananchi wake na kuahidi
kutumia mafunzo hayo vizuri ili kujipatia kipato na kuepukana na dhana
ya kwamba watu wa Dodoma ni ombaomba.
Pamoja na kuwakabidhi vyeti vya
kuhitimu Naibu Waziri Ikupa alifungua pia Soko la Buigiri kwa ajili ya
walemavu hao na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino
kuwaongezea kiasi cha Sh Milioni Tatu ili waweze kukuza mitaji yao.
0 comments:
Post a Comment