Naibu waziri wizara ya kilimo Mhe
Hussein Bashe akiongea na wanaushirika wa wilaya ya Chato hivi karbuni
katika jitihada za kukufua kiwanda cha kuchakata pamba (chato Ginery)
kilichopo wilayani hapo.
Naibu waziri wizara ya kilimo Mhe
Hussein Bashe akikagua shehena ya pamba katika kiwanda cha KOMWE
kilichopo kahama hivi karibuni lengo likiwa kujua namna ambavyo
wananunua pamba ya wakulia.
Naibu waziri wizara ya
kilimo Mhe Hussein Bashe akiangali lebo katika mafuta yalityozalishwa
moja ya chama cha ushirika wilayani hapo.
Na Bashiri Salum,Wizara ya kilimo,Chato
Naibu Waziri Kilimo Mhe. Husseni Bashe leo tarehe 02.10. 2019
amesema Wizara inaandaa mpango wa kutoa zawadi kwa kila kata
itakayofanya vizuri katika kilimo kwa kuongeza uzalishaji na tija.
Watendaji wa Kata na Vijiji ni moja kati ya Viongozi watakao
pata zawadi binafsi kutokana na umuhimu wao katika kukisimamia kilimo
pamoja na masoko ya mazao.
Akiongea wakati wa ziara yake Wilayani Chato Mhe. Naibu Waziri
amesema kwamba Wizara ya Kilimo imeandaa fomu maalumu ambayo itatumika
katika ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wakulima zoezi ambalo
litarahisiha ufuatiliaji wa shuhuli za kilimo.
Mhe. Bashe amesisitiza kwamba fomu hiyo itakayokuwa na taarifa za wakulima zitasaidia kuendeleza kilimo kwa kuwa itaongeza usamamizi kwa viongozi wa kijiji wataalamu wa kilimo na ngazi za watoa maamuzi.
“Kama wizara tutashirikiana na maafisa kilimo ngazi ya wilaya
kuhakikisha kata itakayofanya vizuri itapewa zawadi ambayo bado kwa
ajili ya kata hiyo na zawadi kwa viongozi wote wa kijiji”. Alisema
Bashe.
Fomu hizo zimeandaliwa kupata taarifa kuhusu kwanini mkulima
mwaka uliopita alifanikiwa au hakufanikiwa,alitumia pembejeo zipi za
kilimo kwa mwaka uliopita ambapo maboresho yataanzia hapo alifafanua
Mhe.Bashe.
Aidha katika utekelezaji wake kamati maalumu zitaundwa katika
ngazi ya Halmashauri ambazo zitaandaa vigezo vya kuipata kata iliyofanya
vizuri wakati wizara ikiandaa aina ya zawadi kulingana na aina ya mazao
katika kata husika.
Amesema fumu hizo zitamuwezesha
afisa kilimo na ushirika au mkuu wa wilaya kuwasiliana moja kwa moja na
mkulima na kuhoji juu ya taarifa hizo ambapo ndipo ufuatiliaji utaanzia
hapo.
aidha Mhe. Bashe amesema mfumo huo utasaidia upatikanaji wa taarifa muhimu na mawasiliano
ya moja kwa moja na mkulima hivyo kuondoa tatizo la ukosefu wa taarifa
baina ya serikali na wakulima pamoja na masoko.
Hata hivyo Mhe. Bashe ameziomba
Halmashauri zote nchini kuweka malengo ya uzalishaji wa mazao kwa kila
kila kata sambamba na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao ya wakulima
hasa kipindi hiki ambacho serikali inajitahidi kubadilisha kilimo kutoka
cha kujikimu mpaka kilimo cha kibiashara.
Naye Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika (DAICO) wa Wilaya Chato Bw.Salimu Msuya amemuambia Naibu Waziri kwamba uzalilishaji umekuwa ukipungua maeneo mengi hapa nchini sababu ikiwa ni wakulima wengi kutofuata kanuni bora za kilimo (best agriculture practices) hivyo kuwa na mimea michache katika ekari moja.
“Utakuta mkulima anasema amelima ekari moja lakini kiukweli mimea iliyopandwa ni kidogo(plant population) kwa kutozingatia nafasi sahihi katika upandaji,kama ekari moja ingeingiza mimea 20,000 utakuta mkulima kapanda mimiea 7,000 hawezi kupata tija”Alifafanua Bw.Msuya.
Amesema hali ya uzalishaji katiika kilimo Wilayani Chato
umeongezeka kutokana na wagani kusimiamia upandaji kwa kutumia mistari
zoezi ambalo bado linaendelea.
Hata hivyo Bwana Msuya ameongezea kwamba kutozingati muda katika
kilimo (agriculture timing) ni changamoto kwa wakulima walio wengi
kwani hawalimi kwa na kupanda kwa wakati hivyo kujikuta wamepitwa na
msimu wa kilimo na kusababisha mavuno kuwa kidogo.
Hata hivyo Bwana msuya amemuahidi Mhe Naibu waziri kwamba fomu hizo zitasaidia hata kuwajulisha wakulima kuanza kwa msimu,matumizi ya mbegu bora na utumiaji wa kamba katika upandaji.
0 comments:
Post a Comment