Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kulia) akikagua eneo la
ufukwe la Bondeni Pwani kata ya Kilindoni jana ambalo baadhi ya
wananchi wa Mafia wamelalamika kuzuiwa na mmiliki wake. Wa pili kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Shaib Nnunduma.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akizungumza na wananchi aliowakuta katika ufukwe wa Bondeni Pwani kata
ya Kilindoni jana wakati wa kukagua eneo hilo linalolalamikiwa kuwa
mmiliki wake amekuwa akiwazuia kupita wakati wa ziara yake ya siku mbili
wilayani Mafia.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa nne kulia) akikagua eneo la
ufukwe la Bondeni Pwani kata ya Kilindoni jana ambalo baadhi ya wananchi
wa Mafia wamelalamika kuzuiwa na mmiliki wake. Wa pili kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Mafia mkoani Pwani Shaib Nnunduma na wa tatu kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Mafia Mbaraka Dau.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).
***************************************
Na Munir Shemweta, WANMM MAFIA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
ameitaka halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoa wa Pwani kuandaa mazingira
kupokea uwekezaji wa utalii kwa kupanga na kupima maeneo yake kwa lengo
la kuhamasisha wawekezaji wa sekta ya utalii.
Dkt
Mabula alisema hayo jana kwa nyakati tofauti aliposikiliza kero za
migogoro ya ardhi kwa wananchi wa kata za Baleni na Kilindoni wilayani
Mafia mkoa wa Pawani wakati wa ziara yake ya siku mbili kuhamasisha
ukusanyaji maduhuli ya serikali kupitia kodi ya ardhi, kukagua masijala
ya ardhi pamoja na mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi kwa njia ya
kielektroniki.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisema, eneo la Mafia
limekaa kimkakati na yasipofanyika maandalizi mapema kama vile kupima
maeneo ya uwekezaji basi migogoro ya ardhi haitaisha na hivyo kuwafanya
wawekezaji kushindwa kuwekeza katika wilaya hiyo.
Ameitaka
halmashauri ya wilaya ya Mafia kukusaidia kuweka mipango ya matumizi
bora ya ardhi katika maeneo ya vijiji na kubainisha kuwa mpango huo
unaweza pia kugharimiwa na vijiji husika kwa kuwa gharama yake haizidi
shilingi milioni saba kwa kila kijiji na mpango huo utawezesha
kuandaliwa maeneo ya kilimo, ufugaji na uwekezaji.
‘’Huu
ni mwaka wa uwekezaji Wizara ya Ardhi ni wizara wezeshi tutafanya kila
jitihada kupima viwanja katika eneeo la mafia na Kila anayetaka kuwekeza
anataka Mafia lakini Mafia yenyewe haijawa tayari alisema Dkt Mabula
Kwa
mujibu wa Dkt Mabula, wizara yake iko tayari kuleta timu maalum ya
wapimaji kutoka Wizarani kwa ajili ya zoezi la kupima maeneo mbalimbali
katika wilaya hiyo pale ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya
Mafia atakuwa tayari kugharimia fedha ya kujikimu kwa watumishi
watakaofanya kazi hiyo.
Hata
hivyo, Naibu Waziri wa Ardhi alibainisha kuwa, halmashauri ya Wilaya ya
Mafia inaweza pia kuandika Andiko litakalowezesha halmashauri hiyo
kupata mkopo kwa ajili ya zoezi la upimaji katika maeneo mbalimbali
wilayani humo.
Awali
baadhi ya wananchi wa Mafia wamelalamikia halmashauri ya Mafia kwa
kushindwa kupima maeneo mengi ya wilaya hiyo jambo walilolieleza
limechangia kuwepo migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo. Hata hivyo
changamoto kubwa inayoikabili wilaya ya Mafia ni kuwa na Mtumishi mmoja
wa sekta ya Ardhi.
Maulid
Mjenga alimueleza Dkt Mabula kuwa tatizo la upimaji katika wilaya hiyo
mbali na mambo mengine lakini limesababisha mipaka ya Shule ya Msingi
Kilindoni kutofahamika jambo lililochangia mfadhili aliyejitokeza
kujenga ukuta wa shule kushindwa kufanya hivyo kutokana na kutojulikana
kwa mipaka ya shule.
Migogoro
mikubwa ya ardhi aliyokumbana nayo Dkt Mabula katika ziara yake
wilayani Mafia ni pamoja na mgogoro wa wananchi wenye maeneo na kampuni
ya Bronkhorst International Contractors Limited unaohusu fidia eneo la
Ras Kisimani Mafia, mgogoro wa fidia kati ya kampuni ya Kinasi Lodge na
familia ya Mwanahafsa na Bi Lawiya eneo la Utende pamoja pamoja na ule
wa fidia katika shamba la Utumaini.
0 comments:
Post a Comment